HabariHabari za KauntiHabari za Kitaifa

Wanamtusi mjane, watoto wa Raila, Sifuna akashifu viongozi wa ODM

Na KEVIN CHERUIYOT October 19th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna na baadhi ya viongozi wa Linda Mwananchi wamewakosoa baadhi ya viongozi wa ODM kwa kumkosea heshima mjane wa Raila Odinga, Mama Ida pamoja na familia ya waziri huyo mkuu wa zamani.

Akizungumza katika ibada ya kanisa, eneobunge la Embakasi Mashariki jana, Bw Sifuna alisema kuvurugwa kwa maadhimisho ya kwanza ya kifo cha Raila eneo la Bondo kulipangwa na viongozi wa eneo hilo waliopinga mwaliko wa viongozi wa Linda Mwananchi.

“Watu wale wale waliokuwa wameapa kuwa hawatakula kabla Raila hajatoa maagizo wamemsahau na sasa wanaimba wimbo wa mtu mwengine. Wanamtukana mjane wake na hata watoto wake,” akasema Bw Sifuna.

Bw Sifuna alisema mrengo wake utailinda familia hiyo na kuendeleza maono na uanaharakati wa Raila, ikiwemo kuhakikisha demokrasia. Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino naye aliishutumu serikali kwa kukaa kimya huku ufisadi ukiharibu Jiji la Nairobi.

Aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa gavana, ataboresha barabara, kuhakikisha wanafunzi wanapata busari bila malipo, kusafisha jiji na kuunda nafasi za ajira kwa vijana.