• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
TSC kuwaajiri walimu 1,045

TSC kuwaajiri walimu 1,045

Na WANDERI KAMAU

TUME ya Kuwaajiri Walimu (TSC) imetangaza nafasi 1,050 mpya za walimu zilizoachwa wazi na walimu waliostaafu.

Nafasi hizo zinajumuisha 832 katika shule za msingi na 218 katika shule za upili.

Kwenye tangazo katika vyombo vya habari jana, tume hiyo ilisema kwamba, wale watakaotuma maombi hayo ni walio chini ya miaka 45 na lazima wawe wamesajiliwa nayo.

Wale wanaotuma maombi ya shule za msingi lazima wawe wamefikia kiwango cha P1, huku wale wanaotuma kuomba nafasi za shule ya upili watahitajika kufikisha masomo yao katika kiwango cha diploma.

Tume vile vile ilisema kwamba, kinyume na zamani, ambapo walimu walikuwa wakituma maombi kwake moja kwa moja, mara hii watahitajika kutuma maombi hayo kwa wakurugenzi wa elimu katika kaunti.

Wale wa shule za upili wameagizwa kutuma maombi yao kwa bodi simamizi za shule ambapo nafasi hiyo imetangazwa na nakala nyingine kwa Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti.

Kulingana na tume, hatua hiyo ni awamu ya kwanza ya kuwaajiri walimu zaidi ya 5,000 katika shule za msingi na upili ili kusaidia mpango wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote wanaomaliza shule ya msingi wamejiunga na shule za upili.

Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo, Nancy Macharia (pichani) alisema idadi hiyo itafikisha walimu walioajiriwa kufikia 12,000 tangu mwaka uliopita.

“Walimu hao watasaidia kufanikisha mpango wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote ambao wanamaliza shule za msingi wanajiunga na shule za upili kwa asilimia 100,” akasema Bi Macharia.

Mpango huo utarajiwa kuigharimu serikali Sh3 bilioni.

You can share this post!

Turkana, Baringo na Pokot zalia njaa

Jela maisha kwa kuua shahidi katika kesi inayowakabili

adminleo