• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
JSC yapendekeza jopo libuniwe kumtimua Jaji Ojwang

JSC yapendekeza jopo libuniwe kumtimua Jaji Ojwang

Na RICHARD MUNGUTI

TUME ya Huduma za Mahakama (JSC) imempendekezea Rais Uhuru Kenyatta ateue jopo la majaji kumtimua kazini Jaji Jackton Boma Ojwang huku ombi lingine likiwasilishwa la kufuta kazi Jaji Mohammed Warsame kwa madai ya kupokea hongo ya jumla ya Sh62 milioni.

Tume hiyo ilikuwa imepokea malalamishi dhidi ya Jaji Ojwang kwamba akiwa jaji katika mahakama kuu aliamua kesi ikimpendelea Gavana Okoth Obado alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya Sonny Sugar.

Ilidaiwa Jaji Ojwang alitoa uamuzi uliopendelea kampuni hiyo na ndipo akajengewa barabara ya lami kuenda nyumbani kwake.

Jaji Ojwang hakufika mbele ya JSC kujitetea akidai maamuzi ya mahakama huwa yamelindwa na katiba na hakuna jaji yeyote anapasa kuachishwa kazi kwa sababu ya kutekeleza kazi yake.

Jopo lililotoa uamuzi huo kwamba Jaji Ojwang atimuliwe kwa utovu wa nidhamu na kukaidi mwongozo wa utenda kazi.

Jaji Ojwang aliwatuma mawakili wake kumwakilisha katika jopo hilo lakini akafukuzwa na kuelezwa jaji mwenyewe afike mbele yake na kujitetea.

You can share this post!

Jina langu liondolewe kwa ripoti ya PAC – Monica Juma

Kuna raha zaidi kuishi Somalia kuliko Kenya – Umoja...

adminleo