• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 3:25 PM
SGR kati ya Nairobi na Naivasha kukamilika Juni 30

SGR kati ya Nairobi na Naivasha kukamilika Juni 30

Na BERNARDINE MUTANU

Ujenzi wa reli ya kisasa ya kilomita 120 kati ya Nairobi na Naivasha unakaribia kukamilika na inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Kufikia sasa, asilimia 90 ya ujenzi huo imekamilika, miezi 16 baada ya ujenzi huo kuanza.

Kaimu Meneja Mkurugenzi wa Kenya Railways Philip Mainga alisema kuwa ujenzi wa reli hiyo utakamilika kabla ya siku ya mwisho ya Juni, licha ya mgogoro unaoendelea kuhusua fidia katika eneo kati ya Ngong’ na Rongai.

“Awamu ya 2A kati ya Nairobi-Naivasha imekamilika kwa asilimia 90 na tunaendelea na ujenzi. Tunatarajia kumaliza ujenzi huo kufikia Mei 31,” alisema Bw Mainga.

Alisema kuwa shirika hilo linashirikiana na Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) kutatua mzozo unaoshuhudiwa kuhusiana na fidia ya Sh7.2 bilioni na wamiliki wa mashamba walioathiriwa na ujenzi reli hiyo.

“NLC inatia bidii kulipa Sh7.2 bilioni katika maeneo ya Rongai na Ngong urefu wa kilomita tano. Tunafanya chochote tuwezacho kuhakikisha kuwa pesa hizo zimelipwa ili tuweze kukamilisha mradi huo kwa wakati ufaao,” alisema.

Ujenzi wa reli hiyo utagharimu wananchi Sh150 bilioni ambapo serikali ina lengo la kuunganisha Mombasa na Kampala kupitia Nairobi, Naivasha, Kisumu na Malaba.

Ujenzi wa sehemu hiyo ya SGR umekumbwa mara kwa mara na migogoro. Mwaka jana, wafanyikazi waligoma kwa kulalamika malipo ya chini eneo la Mai Mahiu.

You can share this post!

Kenya pazuri kupata mkopo mwingine wa Eurobond

Prof Magoha aidhinishwa na bunge kuwa Waziri wa Elimu

adminleo