Habari Mseto

Burudani ya kipekee chuoni TUM Purity Nekesa akiibuka mrembo wa mwaka

March 31st, 2019 Kusoma ni dakika: 1

NA STEVE MOKAYA 

JUMA la Maonyesho ya Kitamaduni na Urembo katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM) liliisha  Jumapili asubuhi kwa uchovu kutokana na burudani ya usiku kucha.

Katika sherehe hizo zilizoandaliwa katika uwanja wa chuo hicho, wanafunzi walikesha wakisakata ngoma na kushuhudia vipaji mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wenza pamoja na wasanii kutoka nje.

Kilele cha maonyesho hayo kilikuwa ni kuvishwa taji kwa barobaro mtanashati zaidi na mrembo aliyeumbika zaidi. (Mr&Miss TUM)

Wanaume walishiriki kwa kuinua vyuma na kuonyesha misuli yao, huku mabanati wakishiriki katika mashindano ya urembo  jukwaani.

Hatimaye, William Yuke aliibuka mshindi katika kitengo cha wanaume, huku Purity Nekesa akiwapiku washindani wote katika kitengo cha wanawake. Wawili hao (pichani juu) wanachukua nafasi ya Bwana na Bi TUM katika kipindi cha mwaka 2019/2020.

Mkali wa kibao ‘Landlord, Meja alipowatumbuiza wanafunzi wa TUM, Mombasa Machi 30, 2019. Picha/ Steve Mokaya

Wasanii mbalimbali kwa jumla walikuwa kuyapa maonyesho hayo mvuto na mnato zaidi. Miongoni mwao ni msanii Meja na mvunja mbavu DJ Shiti.

Maonyesho hayo yalihusisha shughuli mbalimbali. Baadhi yazo ni soka, mapishi, na densi za jamii mbalimbali.

Timu mbalimbali zilizoshiriki katika kandanda zilitolewa katika idara mbalimbali. Aidha, makundi mbalimbali ya wanafunzi yailiandaa vyakula vya kiasili na kuviwasilisha katika majaji kwa utathmini na kuzawadiwa alama.

DJ Shiti alifika Pwani kuwachekesha wanafunzi wa TUM. Picha/ Steve Mokaya