• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Mchakato wa uchaguzi wa mawakili warahisishwa

Mchakato wa uchaguzi wa mawakili warahisishwa

Na KENNEDY KIMANTHI

MAWAKILI wamepitisha hoja ya kuondoa mahitaji ya vyeti vya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya (KRA) kabla ya kuruhusiwa kuwania nyadhifa katika Chama cha Mawakili (LSK).

Uamuzi wa kuondoa masharti hayo ulipitishwa kwa kura 287 dhidi ya 190, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanywa Jumamosi jijini Nairobi.

Wagombeaji viti katika LSK watahitajika tu kuwasilisha cheti cha maadili mema na kile cha kuthibitisha usajili wa kikazi.

Wanachama wa LSK walikuwa wametofautiana wakati Wakili Tom Ojienda, ambaye amekuwa akikumbwa na mizozo na KRA, aliporuhusiwa kuwania wadhifa wa mwakilishi wa kiume katika Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), ilhali hana cheti cha kuthibitisha amelipa ushuru ipasavyo kwa KRA.

Uamuzi huo wa Jumamosi umekomesha mgawanyiko mkubwa ambao ulikuwa umetokea katika chama hicho, wakati baraza la LSK lilipobatilisha uamuzi wa kamati ya chama kuhusu wagombeaji wawili wa nafasi katika JSC.

Baraza hilo lilibatilisha pia uamuzi wa Rais wa LSK, Bw Allen Gichuhi kuitisha mkutano wa dharura kujadili uamuzi wa kumruhusu Prof Ojienda na wakili Gathii Irungu kuwania nafasi hizo licha ya ripoti ya kamati iliyowazuia kufanya hivyo.

Wengine wanaomezea mate nyadhifa hizo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA), Bw Macharia Njeru, Bw Alex Gatundu na Bw Charles Mongare.

Hoja hiyo ilikuwa imewasilishwa na wakili Georgiadis Majimbo, ambaye alidai mahitaji ya kutaka wagombeaji wawe na vyeti vya HELB na KRA yamewahi kutumiwa vibaya katika miaka iliyopita.

“Mahitaji hayo mawili yanaweza kutumiwa vibaya na hakika, yamewahi kutumiwa vibaya awali ambapo watu wa nje waliingilia na kutatiza ugombeaji wa wanachama ambao si wandani wao,” akasema Bw Majimbo kwenye ombi lake.

“Mahakama imewahi kutoa uamuzi wake mara nyingi kuhusu suala hili na ikaamuliwa vyeti hivi haviwezi kutumiwa kuamua kuhusu uadilifu wa mtu,” akazidi kusema.

Wanachama watapiga kura Mei kuamua mwakilishi wa kiume atakayewawakilisha katika JSC, ambayo itakuwa na jukumu kubwa la kuchagua majaji watakaochukua mahali pa majaji wawili wa Mahakama ya Juu ambao watastaafu mwaka ujao, na Jaji Mk

You can share this post!

Matapeli wanavyotumia mazishi bandia kulaghai wabunge

Uganda ipewe ardhi lakini kwa mkataba maalum, makuli sasa...

adminleo