• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Wafuasi wa Jehova Wanyonyi washerekea Pasaka bila mungu

Wafuasi wa Jehova Wanyonyi washerekea Pasaka bila mungu

Na TITUS OMINDE

MIAKA minne tangu Jehova Wanyonyi, aliyejitawaza kuwa ‘Mungu’ kufariki na kuzikwa kisiri, wafuasi wa dhehebu hilo wanaamini yu hai na atarudi siku moja kuwachukua.

“Wale wanaofikiri kuwa Jehova Wanyonyi alikufa wanaota. Mungu hafi. Hivi karibuni atarudi hapa Chemororoch,” alisema kuhani mkuu Eliab Masinde ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya mkuu wa dhehebu hilo la Waisraeli Waliopotea.

Mzee Masinde alikemea wanahabari waliodai kuwa Jehova Wanyonyi alifariki. Anadai wanaoeneza uvumi kuwa Jehova alikufa watapatwa na laana.

“Nyinyi waandishi msiwe na tabia ya kutangaza Mungu wetu amekufa. Mnajua twaweza kuamrisha moto uwachome ninyi nyote saa hii,” alionya Bw Masinde, alipoongoza ibada ya Pasaka.

Alisema dhehebu hilo halisherehekei Pasaka kama Wakristo wengine, kwa kuwa wanajua Mungu wao yu hai. “Sisi tunajua mungu wetu alienda safarini na hivi karibuni atarudi. Hii sherehe ni ya kujiandaa kumlaki Jehova hivi karibuni.”

You can share this post!

Vijana wanapeleka hela kwa kamari badala ya kulewa, KBL...

Uhuru aungana na familia ya mzee Moi kuomboleza

adminleo