• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Madaktari wa Cuba wahamishiwa kaunti zingine

Madaktari wa Cuba wahamishiwa kaunti zingine

Na BERNARDINE MUTANU

Madaktari wa Cuba waliokuwa wametolewa kuhudumu katika kaunti tano wameondolewa huko na kupelekwa katika hospitali katika kaunti zingine.

Madaktari hao 10 waliondolewa Isiolo, Tana River, Garissa, Lamu na Wajir na kupelekwa Nairobi na Kiambu katika Hospitali Kuu ya Kenyatta (KNH), Hospitali ya Majeruhi wa Uti wa Mgongo miongoni mwa hospitali zingine Kiambu.

Ingawa kuondoka kwao huenda kukaathiri utoaji wa huduma maeneo hayo, Waziri Msaidizi wa Afya Rashid Aman alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuwahakikishia usalama wao.

“Hii ni hatua ya kiusalama iliyochukuliwa kuhakikisha kuwa madaktari wote wamo salama. Hata hivyo, uhamisho huo ni wa muda. Bado wanatoa huduma za kitaalam kwa sababu bado tunawahitaji,” alisema.

Aliongeza kuwa waliotumwa katika Kaunti ya Kiambu ni madaktari wa familia na wanatoa huduma zao katika zahanati na vituo vya afya.

Serikali ilichukua hatua hiyo baada ya madaktari wawili kutekwa nyara walipokuwa wakihudumu katika Kaunti ya Mandera, mwezi jana.

Dkt Assel Herera Correa, daktari wa jumla na Dkt Landy Rodriguez (mpasuaji) walitekwa nyara na watu waliokuwa wamejiami wakielekea kazini, Afisa wa polisi aliyekuwa akiwalinda aliuawa wakati wa kisa hicho.

Serikali inajitahidi kwa lengo la kuwarai watekaji wao, wanaoaminika kuwa wanamgambo wa al-Shabaab, kuwaachilia.

Sio mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kutekwa nyara na al-Shabaab nchini.

You can share this post!

Familia ya Rai tayari kununua Aquamist

CBK yaonya benki kuhusu wafanyakazi walaghai

adminleo