• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 2:37 PM
AFYA: Manufaa ya kula mananasi

AFYA: Manufaa ya kula mananasi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MWILI unapokosa kinga imara, huwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa kama vile mtu kupata uvimbe yakiwemo majipu au maradhi ya kusababisha muwasho; inflamatory diseases.

Katika kukabiliana na matatizo kama hayo, nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamini nyingi na virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuupa kinga mwili wako dhidi ya magonjwa hayo na mengine.

Umuhimu wa nanasi upo kwenye kirutubisho aina ya “Bromelain” ambacho kinapatikana kwa wingi kwenye tunda hili.

Virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa muhimu sana katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.

Faida nyingine za nanasi ni kama vile:

Usagaji wa chakula

Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo.

Kinga ya mwili

Nanasi linaaminika pia kuwa miongoni mwa matunda yenye Vitamini C kwa wingi ambayo kazi yake ni kuupa mwili kinga dhidi ya “wavamizi” mbalimbali (free radicals), ambao mara waingiapo mwilini, kazi yao huwa ni kuharibu chembechembe hai za mwili.

Vitamini C pia inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Mwili huwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, na maambukizi mengine.

Chanzo cha madini

Mbali ya kuwa ni chanzo kizuri cha Vitamini C, nanasi pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘Manganese’ ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha ufanisi wa vimeng’enyo mbalimbali vya mwili, vikiwemo vya kuzalisha nishati na kinga. tunda hili pia lina kiwango cha kutosha cha Vitamin B1 (Thiamine).

Kuimarisha nuru ya macho

Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho, lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Ulaji wa tunda hili na matunda mengine, huondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho.

You can share this post!

Pep awaonya City watarajie mtihani mgumu msimu ujao

SHANGAZI AKUJIBU: Nimezaa naye ila ni mume wa mtu na ni...

adminleo