• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Marekani yalegeza msimamo wake wa kuizima Huawei

Marekani yalegeza msimamo wake wa kuizima Huawei

MASHIRIKA na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya kutengeneza simu ya Huawei imepata nafuu baada ya serikali ya Marekani kuirahishia vikwazo ilivyoiwekea.

Hatua hiyo inalenga kuwapunguzia udhia watumiaji wa simu za Huawei, kampuni ya China. Hata hivyo, mwanzilishi wa kampuni hiyo alipuzilia mbali hatua hiyo kwa kusema kampuni hiyo ya teknolojia ilikuwa imejitayarishia hatua ya Serikali ya Marekani.

Idara ya Biashara Marekani ilitangaza kuwa itaruhusu Huawei Technologies Co Limited kununua bidhaa zilizotengenezewa Marekani ili kudumisha mfumo wa sasa, na kustawisha mfumo kwa simu zilizotengenezwa na Huawei.

Lakini kampuni hiyo, iliyo kubwa zaidi kwa utengenezaji wa simu bado imezuiliwa kununua sehemu kutoka Amerika kutengeneza bidhaa mpya bila leseni, ambayo huenda ikanyimwa.

Serikali ya Marekani ilisema ilikuwa imewekea Huawei vikwazo kwa sababu kampuni hiyo ilikuwa imekiuka sheria kwa kujihusisha na shughuli kinyume na kanuni za usalama wa kitaifa au sera ya kigeni.

Idhini hiyo ililenga kuyapa makampuni ambayo hutegemea Huawei muda wa kutafuta kampuni mbadala za kushirikiano nazo, alisema Waziri wa Biashara wa Amerika Wilbur Ross, katika taarifa Jumatatu.

“Kwa kifupi, leseni hii itaruhusu operesheni kuendelea kwa watumiaji wa sasa wa Huawei na mfumo wake maeneo ya mashambani,” aliongeza Ross.

Leseni hiyo, ambayo itaendelea kutumiwa hadi Agosti 19 inadokeza kuwa mabadiliko katika utumiaji wa vifaa vya Huawei huenda yakaathiri vibaya wateja wake.

You can share this post!

Kombora nililopiga Leicester ni leseni ya kuondoka Etihad...

Wakenya wanaotamani kusafiri Canada waonywa

adminleo