• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Mzee Wanjigi hafai kuamriwa afike kortini – Mawakili

Mzee Wanjigi hafai kuamriwa afike kortini – Mawakili

Kutoka kushoto: Mawakili Nelson Havi, James Orengo na John Khaminwa wanaowakilisha Mzee Maina Wanjigi katika kesi ya kusumbuliwa na polisi pamoja na mwanawe Jimi Wanjigi. Picha/ Richard Munguti

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Waziri Bw Maina Wanjigi hatafika kortini hivi karibuni kujibu mashtaka  ya kutopata cheti cha umiliki wa silaha.

Jaji  Roselyn Aburili aliamuru mahakama ya Nyeri isiendelee na kesi dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 87 aliyekuwa mbunge wa Kamkunji kwa miongo kadha.

Jaji Aburili alifahamishwa kuwa polisi wamekuwa wakisumbua familia ya Bw Wanjigi na kwamba haki zao zimekiukwa.

Mawakili Kiogora Mugambi , Nelson Havi na John Khaminwa walimweleza Jaji Aburili kwamba Mzee Maina yuko Uingereza akipokea matibabu na kwamba amri afike katika mahakama ya Nyeri kujibu mashtaka hayafai.

Jaji Aburili alikubaliana na mawakili Khaminwa, Havi ,Orengo na Kiongora kwamba wamethibitisha haki za Maina zimekiukwa.

Jaji huyo aliamuru mawakili hao wawasilishe kesi kamili katika muda wa siku 14 ndipo wawasilishe ushahidi kwamba serikali inawasumbua Mzee Maina Wanjigi.

Khaminwa alisema, “Hakuna ukiukaji mwingine wa hali ya juu wa haki za Mzee Maina Wanjigi kama kumweleza afike kortini akiwa mngonjwa.”

Alisema polisi walivamia makazi ya mwanawe mtaani Muthaiga Oktoba 17, 2017 wakidai wanasaka silaha.

Jaji mwingine wa Mahakama kuu George Odunga pia amezima hatua ya kumshtaki Bw Jimi Wanjigi.

You can share this post!

Hata mruke angani, marufuku ya makaa itadumu, aapa Gavana...

Ashangaza kuiba mafuta ya kupikia na sabuni ya Sh17 milioni

adminleo