• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 2:18 PM
Magunia 580 ya sukari ghushi yanaswa Narok

Magunia 580 ya sukari ghushi yanaswa Narok

NA GEORGE SAYAGIE

MAKACHERO mjini Narok Jumanne walinasa magunia 580 ya kilo 90 za sukari yanayoshukiwa kuwa ghushi na kuingizwa nchini kutoka Zambia bila kupitia utaratibu wa uagizaji wa bidhaa kutoka mataifa ya nje.

Mkuu wa DCIO wa Narok Ethiaba Mwenda alisema makachero walikuwa wakipiga doria kama kawaida walipopata sukari ikitolewa kwenye lori na kuingizwa kwenye hifadhi ya duka moja kubwa mjini Narok.

“Mnamo Jumatano jioni, maafisa wetu walipata vidokezo kuhusu magunia 580 ya sukari mjini humo. Kulingana na stakabadhi tulizoona, sukari hiyo iliingizwa nchini kupitia bandari ya Mombasa,” akasema Bw Mwenda.

Sukari hiyo ilkuwa ikihifadhiwa kwenye duka moja maarufu kutoka kwa trela ambayo inaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi unaofanywa na maafisa kutoka Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru(KRA) kwa ushirikiano na makachero ukiendelea.

Afisi ya DCIO vile vile ilitangaza kuwa inaendelea kushirikiana na KRA na Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa(KEBS) ili kubaini kulikotolewa sukari hiyo na iwapo ni sawa kwa matumizi ya raia.

Ingawa hivyo, Bw Mwenda alisema hakuna aliyekamatwa kutokana na kisa hicho japo ukaguzi wa stakabadhi na sukari yenyewe ndio utaamua hatua itakayochukuliwa baadaye.

Aidha afisa huyo aliwaomba wananchi kuwa makini na kupiga ripoti kwa polisi kuhusu trela zinazobeba bidhaa zinazotiliwa shaka ili kuzuia usambazaji wa bidhaa ghushi katika kaunti ya Narok.

“Ningependa kuwaomba umma kushirikiana nasi na kupiga ripoti kuhusu visa vya usafirishaji wa bidhaa wanazoshuku ili hatua ichukuliwe haraka kuzuai usambazaji wa bidhaa hizo,” akasema

You can share this post!

Wanafunzi wana kiu ya kuelewa mimba, hedhi na magonjwa ya...

Mnawaumiza Wakenya kushindia kuongeza bei ya mafuta,...

adminleo