• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 7:55 AM
AFYA: Manufaa ya kula spinachi

AFYA: Manufaa ya kula spinachi

Na MARGARET MAINA na MAJARIDA YA AFYA

[email protected]

SPINACHI ni mboga ambazo huwa laini na za jamii ya sukumawiki.

Fungu la spinachi. Picha/ Margaret Maina

Faida zifuatazo ndizo unaweza kuzipata katika mboga ya spinachi:

Spinachi husaidia kuimarisha afya ya ngozi

Spinachi ina potasiamu kwa wingi, vitamini E na vitamini C ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya ngozi.

Husaidia pia kuilinda ngozi dhidi ya mionzi hatari ya jua kwa watu ambao wanapigwa na jua kwa muda mrefu katika shughuli zao za kila siku.

Husaidia kutibu matatizo mbalimbali ambayo yanahusiana na ngozi ikiwa ni pamoja na chunusi, makovu ya chunusi na shida nyinginezo.

Hii itaweza kusaidiwa kwa kunywa maji ya kutosha kila siku.

Husaidia kuimarisha afya ya macho

Spinachi ina beta-carotene kwa wingi ambayo husaidia macho kuona vizuri. Pia huzuia upungufu wa vitamini A ambayo inahitajika kwa wingi kwa afya ya macho.

Husaidia kuzuia muwasho wa macho au hata kuvimba kwa macho kutokana na uwepo wa virutubisho vingi katika spinachi.

Pia kama una tatizo la kuona hasa usiku, spinachi itakusaidia kupunguza tatitizo hili kama utaiongeza katika milo yako ya kila siku.

Husaidia kuganda kwa damu

Wakati mwingine unaweza kuona umejikata sehemu ndogo tu lakini damu inatiririka kwa kiasi kikubwa na kuchukua muda kusita.

Hii ni dalili ya upungufu wa vitamini K ambayo husaidia kugandisha damu hasa wakati ukiwa umeumia. Kula spinachi kwa wingi kutasaidia hali hii kupungua au kuacha kabisa.

Huimarisha afya ya mifupa

Spinachi ina kiasi kingi cha madini ambayo yana faida nyingi mwilini. Madini hayo ni pamoja na potasiamu, chuma (Iron), manganisi, zinki na shaba (Copper). Madini haya husaidia kuimarisha mifupa na meno.

Kama una tatizo la kucha zako kuwa laini sana na kukatikakatika kila mara, spinachi inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo hili.

Spinachi ina kiwango kikubwa cha protini na ndiyo maana inashauriwa kuliwa kwa wingi ili kuimarisha afya.

Protini ni moja ya vitu muhimu sana katika kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Mwili unapokosa protini huanza kudhoofika na kupoteza nguvu.

Spinachi ni moja ya mboga ya majani zenye virutubisho vingi sana na ina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Kama utaweza kuiongeza katika milo yako kila siku, itakusaidia sana kuimarisha afya yako kwa kiasi kikubwa

Vyakula bora ni dawa tosha kwa miili yetu.

Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini kuna kuhakikishia afya bora na hii itakusaidia sana kupunguza kuingiza kemikali nyingi mwilini unapokuwa unaumwa kwa kutumia dawa.

Mboga hii inaweza kuliwa kwa chakula chochote kama ugali, wali, inaweza pia kutumika kungenezea juisi (smoothie).

Ni nzuri pia kutengezea kachumbari au supu ya mbogamboga.

You can share this post!

AFYA: Umuhimu wa kufanya mazoezi asubuhi

Wafanyabiashara Thika walalama makahaba wamekuwa kero

adminleo