• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Mhadhiri mtafiti wa MKU azidi kutia fora

Mhadhiri mtafiti wa MKU azidi kutia fora

Na LAWRENCE ONGARO

MHADHIRI na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) mjini Thika, Donatus Njoroge, kwa mara nyingine amejizolea sifa baada ya kushinda tuzo nyingine ya kuzuia wadudu kutoeneza uharibifu kupitia teknolojia ya Kibayolojia.

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye hotel moja ya kifahari jijini Nairobi ilikuwa ya kwanza ya International Conference on Agro-Ecology on Transforming Agriculture and Food System in Africa.

Hafla hiyo iliendeshwa chini ya mpango wa World Food Preservation Centre ( IFOAM), Organic International.

Wakati huo pia ulidhaminiwa na washika dau wengine na shirika la Biovision Africa Trust.

Njoroge alikuwa akishindana dhidi ya watafiti wengine 17 kutoka nchi wanachama tofauti kama Kenya, Tanzania, Zambia, Cameroon, Benin, India, Italia, Japan, na Turkey.

Mwongozo wa utafiti huo ulikuwa jinsi ya kupunguza chembechembe fulani kwenye fatalaiza na dawa za wadudu kwa kuongeza uwezo fulani wa kudhibiti uvamizi wa wadudu.

Ubunifu wake umechochea Bw Njoroge kutambulika ulimwenguni kote.

Vilevile hapa nchini ametambuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara.

Mwanakamati

Kutokana na hayo, ameteuliwa kuwa katika kamati kuu ya kutoa mawaidha katika kikundi cha Heckathon cha kutoa maagizo ya serikali kupitia SMEs.

Tuzo nyingine ya mwezi Aprili, ilikuwa ya kimataifa kuhusu ubunifu wa kisayansi na teknolijia ya GIST Tech 1.

Wakati wa kutolewa tuzo hiyo ya awali washika dau wapatao 500 waliwasilisha maombi yao ya Idea Stage na Njoroge ni miongoni mwa wasomi 12 waliofika fainali.

Mwenyekiti wa bodi ya MKU Profesa Simon Gicharu alisema hiyo ni heshima kubwa kwa chuo hicho na watazidi kuwapa usaidizi wahadhiri wenye maono na nia ya kujiendeleza.

Wakati huo pia wanafunzi wapatao 14 wa chuo cha Mount Kenya waliibuka washindi katika maonyesho ya ubunifu wa kiteknolojia.

 

You can share this post!

MWANAMKE MWELEDI: Kidedea katika sekta ya benki

Mwingereza aliyejijengea boma Kakamega azikwa

adminleo