• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 3:03 PM
Wanachama wa Urithi Housing Cooperative washauriwa wawe imara

Wanachama wa Urithi Housing Cooperative washauriwa wawe imara

Na LAWRENCE ONGARO

CHAMA cha Urithi Housing Cooperative Society Ltd kimetoa mwito kwa wanachama wake kuwa imara na kuwekeza nao.

Mwenyekiti wa chama hicho Bw Samuel Maina, alisema aliwahakikishia wanachama wake kuwa wataendelea kuwatumikia kwa unyenyekevu bila ubaguzi wowote.

“Sisi kama chama cha ushirika tutaendelea kuwatumikia wanachama wetu kwa moyo moja bila kuwabagua licha ya changa moto ambazo tumepitia katika siku za hivi karibuni. Tunaelewa kumekuwa na panda shuka za hapa na pale lakini hayo yote tutaweza kuyatatua,” alisema Bw Maina.

Aliyasema hayo mnamo Jumatatu alipofanya mkutano na wanachama wake mjini wa Thika.

Alisema hawezi akakubali chama hicho cha wanachama wapatao 38,000 kiwe na msukosuko wakati kama huu wanapojiandaa kuwauzia ardhi maeneo ya Lamu.

“Ifikapo mwezi Agosti tutawapeleka wanachama wetu kuzuru Kaunti ya Lamu ili kujinunulia kipande cha ardhi katika maeneo hayo,” alisema Bw Maina.

Alisema chama cha Urithi kipo imara kwa lengo la kufuatilia mojawapo za ajenda nne za serikali ya kujenga nyumba kwa Wakenya.

Wanachama waliohudhuria hafla hiyo kwa kauli moja walikubaliana kuwa watazidi kushikana pamoja ili kukuza chama hicho kisisambaratike.

Kuwasilisha

Alisema kwa wakati huu tayari wamejenga nyumba 1,000 ambazo wamewasilisha kwa wanachama kupitia fedha zao za hazina.

Wakati huo pia alisema wamewakabithi wanachama wao vyeti vya umiliki zipatazo 6,000.

Alisema miradi mingine inayoendelea kukamilika inapatikana katika maeneo ya Witeithie, eneo la Juja, Nyumba Mia Project eneo la Rongai, na Osteen Terrace Garden eneo la Joska, ambazo zinatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa 2019.

Alisema lengo kuu la chama hicho ni kuona ya kwamba kinaunganisha Wakenya wote pamoja kwa kuwauzia ardhi kila pembe ya nchi.

Afisa mkuu wa wa vyama vya ushirika Thika Magharibi Bi Catherine Mbuki aliwashauri maafisa wakuu wa chama hicho kufanya juhudi kuona ya kwamba wanakiimarisha chama hicho cha Urithi na kuhakikisha maisha ya wanachama hao inanawiri.”

“Ningetaka kuona mkiendeleza chama hiki kwa uwazi na uwajibikaji ili mwanachama aweze kujivunia matunda ya akiba yake,” alisema Bi Mbuki.

You can share this post!

Voliboli: Kenya yafaa kujiandaa upya kabla ya African Games

Mgonjwa aliyegundulika kuugua Ebola mjini Goma afariki

adminleo