• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Dhamana ya Sh30m kwa Rotich na Thugge au Sh100m pesa taslimu

Dhamana ya Sh30m kwa Rotich na Thugge au Sh100m pesa taslimu

SAM KIPLAGAT Na BENSON MATHEKA

WAZIRI wa Fedha, Henry Rotich na Katibu wa wizara hiyo Kamau Thugge, Jumanne waliachiliwa kwa dhamana ya Sh50 milioni au Sh15 milioni pesa taslimu kila mmoja.

Hii ni baada ya wawili hao kukanusha mashtaka ya ufisadi kuhusiana na sakata ya mabwawa ya Arror na Kimwerer.

Pia waliagizwa wasikanyage ofisi zao na iwapo lazima wafike waandamane na maafisa wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI).

Wawili hao walifikishwa katika mahakama ya ufisadi jijini Nairobi na kushtakiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ya kutumia vibaya mamlaka yao na kutekeleza uhalifu wa kiuchumi.

Katibu wa Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt Susan Koech, ambaye pia alishtakiwa kuhusiana na sakata hiyo, aliachiliwa kwa dhamana ya Sh30 milioni au alipe Sh6 milioni pesa taslimu.

Bw Rotich, Bw Thugge na Dkt Koech walikuwa miongoni mwa watu 24 wanaokabiliwa na mashtaka kuhusu sakata hiyo, ambayo wapelelezi wanasema serikali ilipoteza mabilioni ya pesa.

Mashtaka mengine yanayowakabili ni kukiuka sheria za ununuzi kwa kutoa tenda ya bima kwa miradi hiyo na kuidhinisha malipo kinyume cha sheria.

Walikamatwa Jumatatu pamoja na maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Ustawi wa Bonde la Kerio (KVDA) na Shirika la Kutunza Mazingira (NEMA) kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Mashtaka Noordin Haji na wakalala seli za polisi.

Mkurugenzi Mkuu wa Nema, Geoffrey Wahungu aliachiliwa kwa dhamana ya Sh750,000 pesa taslimu.

Washtakiwa pia waliagizwa wawasilishe paspoti zao kortini, kutofika katika ofisi zao bila kuandamana na wapelelezi na kutotisha mashahidi.

Jana, walipofikishwa mahakamani asubuhi, walifungiwa katika seli za mahakama wakisubiri kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu, Douglas Ogoti.

Upande wa mashtaka uligawa kesi mara nne huku za miradi ya mabwawa ya Arror na Kimwerer zikiwa katika faili tofauti.

Kesi zinazowakabili maafisa wa kamati ya kutoa zabuni katika KVDA zilikuwa katika faili tofauti na za maafisa wa Nema nazi zilikuwa katika faili tofauti.

Kupitia mawakili wao, washukiwa waliomba mahakama iwaachilie kwa dhamana wakisema watakuwa wakifika kortini wakati wa kusikilizwa kwa kesi.

Mawakili Kioko Kilukumi, Kipchumba Murkomen na Philip Nyachoti walisema akukuna na sababu za kufanya mahakama iwanyime dhamana.

You can share this post!

Walimu wataka maeneo ya kunyonyesha

Maraga awashauri magavana na wabunge kujadiliana kwanza

adminleo