• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 3:17 PM
Niachilie nikawapikie watoto, mama amlilia hakimu katika shtaka la wizi

Niachilie nikawapikie watoto, mama amlilia hakimu katika shtaka la wizi

Mary Polyne Khagali (kushoto) na Aquinata Imbwaka wakiwa kizimbani Jumatatu waliposhtakiwa kwa kufanya njama za wizi wa Sh3 milioni kutoka Benki ya Jamii Bora. Picha/RICHARD MUNGUTI

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE aliiyeshtakiwa Jumatatu kwa kufanya njama za kuibia benki ya Jamii Bora Sh3,088,000 Jumatatu aliomba aachiliwe kwa dhamana “akapikie watoto.”

Mary Polyne Khagali  na Aquinata  Imbwaka walifikishwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi na kusomewa mashtaka manne.

Shtaka la kwanza lilikuwa la kufanya njama za kuibia benki hiyo Sh3,088,000. Aquinata alikana aliiba Sh600,000 .

Alikabiliwa na shtaka lingine la kuweka katika akaunti yake  Sh840,000 akijua zimeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

Naye Mary Khagali alikana alikutwa ameweka katika akaunti yake Sh740,000 akijua zimeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

“Naomba uniachilie kwa dhamana nikawapikie watoto wangu, mheshimiwa. Tangu niwekwe korokoroni sijui hata yule mchanga anakula nini. Waonee wanangu huruma na uniachilie kwa dhamana,” alirai Aquinata.

Andayi aliwaachilia kwa dhamana ya Sh200,000 pesa tasilimu kila mmoja.

Kesi itasikizwa Aprili 23.

You can share this post!

Onyo kwa wanaosafirisha mafuta chafu

Washtakiwa kuunda nakala feki za kandarasi za mamilioni

adminleo