• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 1:51 PM
VIDUBWASHA: Utaweza kujipima macho ukiwa nyumbani (The EyeQue VisionCheck)

VIDUBWASHA: Utaweza kujipima macho ukiwa nyumbani (The EyeQue VisionCheck)

Na LEONARD ONYANGO

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa zaidi ya watu 1.3 bilioni wana shida ya macho duniani.

Watu milioni 89 wana matatizo madogo madogo ya macho. Watu milioni 217 wana matatizo makubwa na watu milioni 36 ni vipofu.

WHO inasema kuwa asilimia 80 ya matatizo ya macho yanaweza kuepukika.

Inapendekeza watu wapimwe macho kila baada ya mwaka mmoja ili kuepuka upofu unaoweza kuepukika.

Sasa wataalamu wa matibabu nchini Amerika wamezindua The EyeQue VisionCheck kinachokuwezesha kujipima macho ukiwa nyumbani.

Umbali si hoja

Kifaa hicho pia kinawezesha daktari wa macho kupima mgonjwa bila kuwa karibu naye.

Kadhalika, kinakushauri kuhusu aina ya miwani unayofaa kuvalia unapokuwa na matatizo ya macho bila ushauri wa daktari.

Kifaa hiki kinatumia programu (app) kukutumia matokeo katika simu kwa njia ya Bluetooth.

Kwa vijana wanaovalia miwani ili kuonekana nadhifu, kifaa hiki pia kinawafaa kwani kinawashauri aina ya miwani inayowafaa.

You can share this post!

ITASALIA NDOTO: Neymar kuendelea kupiga soka nchini Ufaransa

SHINA LA UHAI: Nasuri ya Uzazi yawanyima kina mama starehe

adminleo