• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
Mbunge awakejeli magavana waliorudishia serikali mabilioni

Mbunge awakejeli magavana waliorudishia serikali mabilioni

Na Charles Lwanga

MBUNGE wa Kilifi Kaskazini, Bw Owen Baya amewataka magavana wawajibike kutokana na ripoti kuwa baadhi ya kaunti zilirudisha mabilioni ya pesa katika mwaka wa fedha uliopita kwa kukosa matumizi.

Bw Baya (pichani) amewataka magavana kutumia pesa walizopewa na Serikali Kuu kwanza kuletea wananchi maendeleo badala ya kupigania kuongezwa mgao wa pesa.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 35 katika shule ya Upili ya Wasichana ya Ngala Memorial, Dabaso, mbunge huyo alitoa mfano wa kaunti ya Kilifi ambayo alidai kuwa ilikosa kutumia Sh1.74 bilioni na ikalazimishwa kuzirudisha kwa serikali kuu.

“Uongozi wa Kaunti ya Kilifi ulikosa kutumia Sh1.7 bilioni ambazo bado ziko katika akaunti ya serikali ya kaunti licha ya kuwa na miradi ambayo haijakamilika na barabara mbovu,” alisema.

Bw Baya aliuliza ni kwa nini kaunti ambayo inapokea zaidi ya Sh10 bilioni ilikosa kutumia fedha kuleta maendeleo wakati wakazi wanateseka kutokana na barabara na madarasa mabovu.

 

You can share this post!

Serikali kuu idhibiti kisiwa cha Migingo kuzuia ghasia...

Kipusa awaka kupata sketi kitandani

adminleo