• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
Kikosi cha Chipu kwenye raga za Namibia chatajwa

Kikosi cha Chipu kwenye raga za Namibia chatajwa

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imetaja kikosi cha Chipu (chipukizi) kitakachocheza kwenye Raga za Afrika za ukanda wa Kusini za wachezaji wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 nchini Namibia.

Kocha Paul Odera amejumuisha wachezaji wanne wanaosakata raga katika mataifa ya kigeni. Wachezaji hao ni Mark Mutuku (Chuo Kikuu cha Canterbury, New Zealand), Michele Brighetti (Sedbergh School, Uingereza), Jeff Mutuku (Kingswood College, Afrika Kusini) na Andrew Siminyu kutoka Hillcrest School mjini Durban, Afrika Kusini.

Xavier Kipng’etich Bett (Impala Saracens) na Stanley Isogol (Homeboyz) wameteuliwa kuwa nahodha na naibu wa nahodha, mtawalia.

Chipu, ambayo ilimaliza ya pili barani Afrika nyuma ya Namibia mwaka 2013, 2014, 2016 na 2017, itaondoka nchini Machi 26.

Itaanza kampeni yake dhidi ya Madagascar hapo Machi 28 jijini Windhoek. Fainali ya ukanda wa Kusini itakutanisha mshindi kati ya Kenya na Madagascar na mshindi kati ya mabingwa watetezi Namibia, ambao wameshinda mataji manane tangu raga hizi zianzishwe mwaka 2007, na mabingwa wa mwaka 2009, 2010 na 2011 Zimbabwe.

Mshindi wa Afrika ya Kusini atapigania tiketi ya kuwakilisha Afrika katika mashindano ya World Trophy dhidi ya mshindi wa Afrika ya Kaskazini (Tunisia, Morocco, Ivory Coast na Senegal).

Kikosi cha Chipu kitakachosafiri: Joshua Matasi (Impala Saracens), Toby David Francombe (Nondescripts), James Simiyu (Strathmore Leos), William Diffu (Homeboyz), Emmanuel Silungi (Homeboyz), Stanley Isogol (Homeboyz, nahodha msaidizi), Akuei Monate (Nakuru), Mark Mutuku (Chuo Kikuu cha Canterbury, New Zealand), Xavier Kipnge’tich Bett (Impala Saracens, nahodha), Michele Brighetti (Sedbergh School, Uingereza),

Joshua Macharia (KCB), Zeden Marrow (Homeboyz), Victor Matiko (Menengai Oilers), Jeff Mutuku (Kingswood College, Afrika Kusini), Edmund Anya (Strathmore Leos), Kevin Kerore (Mwamba), John Daniel Gichuhi (Homeboyz), Bonface Ochieng (Kenya Harlequins), Harold Anduvate (Menengai Oilers), James McGreevy (Hillcrest School, Nairobi),

Andrew Siminyu (Hillcrest School, Durban, Afrika Kusini), Bethuel Anami (Strathmore Leos), Samuel Asati (KCB), Lucas Oppal (Strathmore Leos), Massimiliano Brighetti (hana klabu).  Vizibo vya majeruhi: Dennis Lusweti (USIU), Allan Aziz (Menengai Oilers), Derrick Keyoga (Menengai Oilers). Benchi la kiufundi – Paul Odera (Kocha Mkuu), Jimmy Mnene (Meneja wa Timu), Stella Mwende (Daktari), Michael Aung (kocha wa washambuliaji), Edwin Boit (kocha wa mazoezi ya viungo).

Ratiba ya Chipu:

Machi 26 – safari ya kuelekea Namibia

Machi 28 – Kenya vs. Madagascar

Machi 31 – Mshindi kati ya Kenya na Madagascar dhidi ya mshindi kati ya Namibia na Zimbabwe

Aprili 1 – safari ya kurejea Kenya

You can share this post!

‘Pocket Rocket’ ajiuzulu mbio za New York City...

Super 8 yaanza wakali wakilemewa na limbukeni

adminleo