• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kuteua ‘mipango ya kando’ kwa afisi za serikali ni uhaini – Kuria

Kuteua ‘mipango ya kando’ kwa afisi za serikali ni uhaini – Kuria

Na MWANGI MUIRURI

MBUNGE wa Gatundu Kusini Moses Kuria Jumatatu amesema kuwa kukiri kwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kuwa alimteua Anne Thumbi kama Diwani Maalum kwa msingi wa urafiki kwa marehemu Ken Okoth ni ishara tosha kuwa nyadhifa hizo zinafaa kutupiliwa mbali.

“Tumepata ukweli halisi kuhusu jinsi magavana hutumia mamlaka yao kutekeleza teuzi afisni kwa madiwani maalum. Sasa tunajua hawa wengi maalum afisini kwa sasa aidha ni jamaa, marafiki au washirika wa magavana,” akasema.

Akiwa Mjini Sagana, Bw Kuria aliteta kuwa “huu ni utapeli mkuu ambapo mtu binafsi anahidfadhi wandani wake ndani ya kapu la pato la kitaifa….”

Alisema kuwa ni sawa na uhaini kwa “mwanamume achukue rafiki wake wa kike akiwa rafiki tu au mpango wa kando na amweke katika ufadhili wa mlipa ushuru.”

Alisema kuwa Sonko tayari amejiangazia kama aliyeshawishika kutapeli Wakenya kupitia kumteua Bi Ann Thumbi kama shukrani ya urafiki yake (Sonko) na marehemu Ken Okoth ambaye inadaiwa alikuwa mpenziye.

“Sasa, tumeambiwa na Sonko kuwa Bi Thumbi ni diwani maalum sio kwa msingi wa uwezo au umakinifu wa kumfaa mwananchi wa Nairobi na huduma za kiutawala bali ni kwa msingi kuwa ni jiko kwa marafiki wa kisiasa,” akasema Kuria.

Alisema kuwa msingi wowote wa kuandaa referenda hapa nchini ukiwa hauna kipengee cha kutupilia mbali “nyadhifa za bure kama hizi za wabunge, maseneta na madiwani maalum, basi hiyo si referenda na inafaa kukataliwa na wote.”

Alisema kuwa “hii ni hali sawa ya punda amechoka kubebezwa mizigo hata ya urafiki wa kitanda, wa kibiashara na kisiasa.”

You can share this post!

Wazee wataka mkewe Ken Okoth ‘arithiwe’...

Jaji Ojwang’ arejeshwa kazini

adminleo