• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Wanasiasa mashuhuri miongoni mwa wanyakuzi wa ardhi Mau

Wanasiasa mashuhuri miongoni mwa wanyakuzi wa ardhi Mau

JOSEPH OPENDA na GEORGE SAYAGIE

VIONGOZI wa kisiasa, maafisa wa ranchi na familia za wanasiasa mashuhuri wametajwa kwenye orodha ya watu wanaoshukiwa kunyakua sehemu ya ardhi ya msitu wa Mau kinyume cha sheria.

Kwenye orodha hiyo iliyochapishwa na serikali magazetini wiki iliyopita, jumla ya watu 600 wameorodheshwa kama wanaomiliki ardhi katika sehemu ya msitu huo ulioko katika kaunti ya Narok na wana vyeti vya kumiliki ardhi walizopata kinyume cha sheria.

Wizara ya Ardhi na Mpango wa Miji sasa inapanga kufutilia mbali vyeti hivyo.

Uamuzi wa serikali kuchapisha orodha ya majina ya watu hao inafuatia amri iliyotolewa na Mahakama ya Mazingira na Ardhi ya Nakuru iliyotolewa mnamo Juni 10. Mahakama hiyo iliagiza serikali ifawahamishe watu hao kuhusu nia yake ya kuharamisha vyeti hivyo.

Hata hivyo, Taifa Leo imepata habari kwamba orodha iliyochapishwa inajumuisha watu wa familia za wanasiasa wenye ushawishi mkubwa na wamiliki wa ranchi ambao wanamiliki sehemu kubwa ya ardhi ambayo serikali inapanga kutwa.

Miongoni mwa waliofaidi kutoka na utoaji wa ardhi ya msitu wa Mau kinyume cha sheria ni; Ololarusu Investment Farm walipewa hekta 4,001 ya ardhi, diwani wa zamani Koremo Ole Surum (hekta 2,988), Francis Lemiso Kipturkut (hekta 2,653) na Ilngina Contractors (hekta 1,295) kampuni inayomilikiwa na mtu wa familia ya aliyekuwa Seneta wa Narok Stephen Ole Ntutu.

Wiki iliyopita, kundi la wanasiasa 15, wengi wao kutoka jamii ya Kalenjin, walikutana Nakuru kwa mazungumzo kuhusu namna na kukabiliana na serikali kuhusu suala hilo.

la ufurushaji wa watu wanaomiliki ardhi katika msitu wa Mau kinyume cha sheria.

Viongozi hao waliongozwa na Seneta wa Baringo Gideon Moi, Gavana wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos, alisema Gavana wa Bomet Isaac Ruto na mbunge maalum Wilson Sossion. Viongozi hao waliitaka serikali kuitisha mazungumzo ili kujadili njia za kushughulikia suala hilo bila kuzua vurugu.

Walilalamika kuwa mpango wa serikali wa kuwafurusha watu kutoka kutoka msitu wa Mau utawacha familia nyingi ambazo zimekuwa zikiishi hapo tangu zamani, bila makao.

Bw Rukuti Ole Koriata, ambaye ni kakake aliyekuwa chifu mkuu Daniel Ole Koriata aliyehudumu wakati wa utawala wa Kanu, pia ni mmoja wa waliorodheshwa kumiliki stakabadhi haramu ya umiliki ardhi.

You can share this post!

Madaktari na wauguzi wakaa ngumu wagonjwa wakifa

Kaunti yatakiwa kubuni sera ya kupunguza chokoraa jijini

adminleo