• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
Matiang’i azimwa kumtawaza chifu aliyepata ‘D’ kwa KCSE

Matiang’i azimwa kumtawaza chifu aliyepata ‘D’ kwa KCSE

Na Richard Munguti

WAZIRI wa Usalama, Dkt Fred Matiang’i, ameagizwa na Mahakama Kuu asitishe uteuzi wa Chifu wa Lokesheni ya Sarmani katika Kaunti ndogo ya Mandera Kaskazini kusubiri uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na wazee 20 wanaodai aliyeteuliwa hajahitimu.

Jaji Byram Ongaya alimwagiza Dkt Matiang’i kusitisha shughuli ya kumtawaza Bw Mohammed Ibrahim Ali, aliyeteuliwa Agosti 20, 2019 kuwa chifu wa Lokesheni ya Sarmani.

Wakili Bonbegi Gesicho aliyewasilisha kesi hiyo alieleza mahakama kwamba kufuatia tangazo la kuteuliwa kwa Bw Ali, mizozo ilichipuka na koo mbali mbali kukabiliana.

“Mali iliteketezwa, nyumba kubomolewa na watu wengi kujeruhiwa kufuatia tangazo la kuteuliwa kwa Ali kuwa Chifu wa Sarman,” bw Gesicho aliambia mahakama.

Alisema Bw Ali hajahitimu kwa kuwa alikuwa na alama ya D katika mtihani wa kidato cha nne na anayehitimu anapaswa kuwa na alama ya C.

“Naomba usitishe uteuzi wa Bw Ali kuepusha maafa zaidi Mandera Kaskazini,” alisema Bw Gesicho.

 

You can share this post!

‘Ndoa ya UhuRuto ilivunjika kitambo’

Aliyeiba kanisani afariki kizuizini

adminleo