• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Moroto apendekeza KRA ikusanye ushuru katika kaunti

Moroto apendekeza KRA ikusanye ushuru katika kaunti

Na OSCAR KAKAI

MBUNGE wa Kapenguria Bw Samuel Moroto ametoa wito kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini (KRA) ichukue jukumu la kukusanya ushuru katika serikali za kaunti, ili kuimarisha ukusanyaji na kuziba mianya za ufisadi.

Alisema kuwa ukusanyaji ushuru umeathirika ambapo hamashauri ya KRA inakosa fedha na kaunti nyingi hazijatimiza kiwango ambacho kinastahili na huwa hazipeana fedha ambazo zimekusanya.

Mbunge huyo alisema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa uwazi kwenye serikali za kaunti ili kulinda fedha za mlipa ushuru.

Bw Moroto alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kumaliza kupotea kwa fedha, matumizi ya juu ambayo huletwa na serikali za kaunti kwenye ukusanyaji ushuru.

Akiongea jana katika kanisa katoliki la Makutano Bw Moroto alisema kuwa magavana wanatumia vibaya na kufuja fedha ambazo wanakusanya suala ambalo limeathiri uchumi wa nchini.

“Jukumu hilo linafaa kupeanwa kwa KRA. Mkurungenzi wa mashtaka ya umma na idara ya upepelezi (DCI) na mkaguzi mkuu wamejaribu kumaliza ufisadi kwenye kaunti. Magavana wanataka fedha nyingi ilihali wakenya wanaumia.Hakuna miradi ya maana inatekelezwa na serikali za kaunti,” akasema Bw Moroto.

Bw Moroto alitoa wito kwa magavana nchini kuwaajibikia fedha ambazo wamekuwa wakikusanya tangu waingie afisini akisema kywa fedha wanafaa kutumia fedha ambazo wao hupewa kabla ya kuitisha zingine.

“Wasimamizi wa kaunti wanakusanya fedha nyingi na kuzifuja. Asilimia ya fedha zinazotoka kwenye kaunti hadi kwenye hazina ya kitaifa ni kidogo sana. Watu ambao hawakuwa hata na baisekeli sasa wanaendesha magari mkubwa kama Brado na wanamiliki mijengo ya maorofa,” alisema.

Mbunge huyo sasa wanawataka magavana ambao wametajwa kwenye ufisadi ya fedha za ukusanyaji ushuru kujiuzulu ama kukaaa kando.

You can share this post!

Wizi wa Sh72m: Korti kufanya maamuzi

SHINA LA UHAI: Changamoto za kulea mtoto aliye na mtindio...

adminleo