• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
UDURUSU WA KCSE: Uchambuzi wa maudhui katika tamthilia ‘Kigogo’

UDURUSU WA KCSE: Uchambuzi wa maudhui katika tamthilia ‘Kigogo’

Na WANDERI KAMAU

BAADHI ya maudhui makuu yaliyo katika tamthilia ‘Kigogo’ ni pamoja na: Uongozi mbaya, dhuluma, uzalendo, nafasi ya mwanamke, migomo, utabaka kati ya mengine.

Uongozi mbaya

Mhusika Ashua, ambaye ni miongoni mwa watu wa tabaka la chini anasema kuwa viongozi katika jimbo la Sagamoyo, chini ya mtawala Majoka wanawadhulumu wanyonge.

“…na kuhangaishwa na wenye nguvu ndio hewa tunayopumua huko.” (uk 2).

Katika jimbo hili, wachochole wanageuzwa watumwa na viongozi walio mamlakani. Kwa mfano, Kombe, Boza na Sudi wanafanya kazi ya kuchonga vinyago vya mashujaa kwa ajili ya sherehe za uhuru.

Viongozi wanatangaza wakati mrefu wa kusherehekea uhuru huku Wanasagamoyo wakiteta vile wanavyoteseka na kudhulumiwa, hasa katika soko la Chapakazi.

Majoka anafadhili mradi wa kuchonga vinyago ambao hauna manufaa yoyote, huku wakazi wakilazimishwa kuulipia, licha ya kukumbwa na hali ya njaa (uk11).

Dhuluma

Majoka anaibuka kuwa kiongozi katili, anayewatesa raia kutokana na miongozo potoshi anayopewa na mshauri wake mkuu, Bw Kenga kuhusu njia za kuwakabili na kuwanyamazisha wapinzani wake.

Hata hivyo, kauli hiyo inapingwa na baadhi ya watu waliokuwa wamechoshwa na maovu ya Bw Majoka.

Watu hao wanaongozwa na mhusika Sudi, Tunu, Siti kati ya wengine.

Wanahisi njama ya hila, jambo linaloibuka kuwa kweli, kwani mpango uliopo ni kulifunga soko ili kumruhusu Majoka kujenga hoteli kubwa ya kisasa.

Maovu mengi yanayoendelezwa ni pamoja na migomo ya wafanyakazi muhimu kama madaktari kwa kutolipwa mishahara yao. Walimu pia wanagoma wakiwa likizoni wakilalamikia mishahara duni (uk35).

Unyakuzi wa ardhi, ufisadi, uzandiki, uhatinafsi, hadaa kati ya maovu mengine ndiyo yanajitokeza kuwa mihimili mikuu ya uongozi wa Majoka.

Uzalendo

Licha ya changamoto wanazopitia, wananchi wa Sagamoyo wanaonyesha uzalendo mkubwa kwa jimbo lao.

Wanalipa kodi kikamilfu kuleta maendeleo licha ya kulaghaiwa.

Katika enzi ya ukoloni, mashujaa walijitolea mhanga ili wavune matunda baada ya uhuru (uk 4).

Wimbo unaoimbwa katika rununu ni wa kizalendo kuonyesha kuwa Wanasagamoyo wanalipenda jimbo lao la Sagamoyo (uk 5).

Sudi anaelewa kuwa uongozi wa Majoka haufai. Anawaeleza Boza na Kombe kuhusu umuhimu wa kuandika upya historia ya Sagamoyo. Kinyago anachokichonga Sudi ni cha shujaa halisi wa Sagamoyo. Anaelewa kuwa Tunu ndiye anayepaswa kuwa kiongozi halisi.

Tunu ni mzalendo katika taifa lake. Anasema kuwa jukumu lake ni kulinda uhai, haki na uhuru. Amejitolea kwa vyovyote kulinda haki Sagamoyo hata ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha yake. Akiwa na wenzake wanaomuunga mkono, anaeleza kuwa amejitolea kuhakikisha kuwa kila Mwanasagamoyo amepata haki (uk 18).

Akiwa mwanafunzi katika chuo kikuu, walipambana wakiwa viongozi wa chama hicho hadi wakaleta mafanikio.

 

Baruapepe ya mwandishi: [email protected]

(MAKALA KUENDELEA)

You can share this post!

KINA CHA FIKIRA: Tafsiri za kizuzu adui mkubwa wa lugha ya...

Wasiwasi wakumba familia baada ya mzee kupotea

adminleo