• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Afueni kwa serikali za kaunti baada ya Kemsa kukubali kuzipa dawa kwa mkopo

Afueni kwa serikali za kaunti baada ya Kemsa kukubali kuzipa dawa kwa mkopo

Na CHARLES WASONGA

KERO ya uhaba wa dawa katika hospitali za umma katika kaunti sasa huenda ikapungua.

Hii ni baada ya Mamlaka ya Usambazaji Dawa Nchini (Kemsa) kulegeza kamba na kuziruhusu serikali za kaunti kuendelea kuagiza dawa na vifaa vingine vya matibabu japo inazidai deni kubwa.

Afisa Mkuu Mtendaji wa mamlaka hiyo Jonah Manjari jana aliwaambia maseneta kwamba kufikia wakati huu, wanadaiwa serikali za kaunti jumla ya Sh2.4 bilioni ambazo ni malimbizi ya kipindi cha miaka mitatu.

“Lakini licha ya deni hili kubwa, milango yetu ingali wazi na tuko tayari kuzipa serikali za kaunti dawa na vifaa vinginevyo vya matibabu kwa mkopo. Hii ni kwa sababu wajibu wetu mkubwa kama asasi ya serikali ni kuokoa maisha wala sio kuchuma faida,” Dkt Manjari akasema alipofika mbele ya kamati ya seneti inayochunguza madai ya ufujaji wa fedha katika mpango wa usambazaji wa mitambo ya matibabu (MES) kwa serikali za kaunti.

Hata hivyo, afisa huyo alisema kaunti kama Narok na Nairobi ambazo zilikuwa zikidaiwa kiasi kikubwa cha fedha tayari zimeanza kulipa madeni yao.

“Kaunti ya Narok imemaliza kulipa deni lake la Sh379 milioni huku Nairobi ikisalia na Sh60 milioni kati ya Sh300 milioni ambazo inadaiwa na Kemsa,” Dkt Manjari akasema.

You can share this post!

IEBC yathibitisha kupokea sahihi za kutaka serikali ya...

Polisi afyatua risasi hewani mtihani ukiendelea

adminleo