• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
MENAA yamtuza Mkenya

MENAA yamtuza Mkenya

Na MAGDALENE WANJA

SHIRIKA la Utoaji Tuzo la Mashariki ya Kati, Afrika ya Kaskazini na Asia (MENAA), limemtuza Mkenya Dkt Mohamed Bahaidar katika tuzo ya kila mwaka ya Best Personal Brand Award.

Kulingana na waandalizi wa tuzo hiyo, Dkt Bahaidar alituzwa kwa juhudi zake za kutafuta suluhu kwa mambo yanayosumbua maishani.

Dkt Bahaidar ambaye ni mzaliwa wa Mombasa ndiye mshindi wa kwanza kutoka nchini Kenya kupokea tuzo hiyo ambayo ndiyo ya kipekee katika Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini.

Dkt Bahaidar ana shahada ya uzamifu katika maswala ya Filosofia ya Usimamizi (Philosophy in Management).

“Ni kutokana na udadisi wake na miaka 14 na utafiti katika maswala ya falsafa ambao umemwezesha kutoa suluhisho kwa zaidi ya maswala 10,000 ya kifamilia,” ilisoma habari hiyo.

Katika mahojiano na Taifa Leo kabla ya kupokea tuzo hiyo, Dkt Bahaidar alisema kuwa alijivunia kupokea ushindi huo katika tuzo hiyo ya kipekee.

“Sikutarajia tuzo hiyo wala sikujua kwamba kuna tuzo kama hii. Ilinibidi nimtume rafiki yangu katika eneo la Oman kubaini kama ni kweli,” akasema Dkt Bahaidar.

Badhi ya vitabu vyake ambavyo vimemfanya kupokea tuzo hii ni pamoja na ‘The Hidden Self’, ‘The Point of Deflection’, ‘A Household of Bliss’, ‘Mirror Reflection’ na ‘Sparkling Hope’.

You can share this post!

Miili ya watatu waliouawa yapatikana imetupwa kijijini Rwera

Mabao ya Rashford yazamisha Chelsea

adminleo