• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
IEBC yajitetea kuhusu sajili ya wapigakura Kibra

IEBC yajitetea kuhusu sajili ya wapigakura Kibra

Na MAUREEN KAKAH?

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumanne alieleza mahakama kwamba imetoa habari zote muhimu kuhusu sajili ya wapigakura katika eneobunge la Kibra ambalo litakuwa na uchaguzi mdogo Alhamisi.

IEBC ilikuwa ikijibu kesi iliyowasilishwa na chama cha ODM.

Ilisema kwamba ni wapigakura wenyewe ambao wanaruhusiwa kisheria kuthibitisha usajili wao wala jukumu hilo sio la vyama vya kisiasa.

Tume hiyo ilisema habari zilizoko kwenye sajili ya wapigakura zinaweza kuthibitishwa na watu wenyewe kwa kuwa stakabadhi za kila mpigakura haziwezi kuanikwa hadharani kwa umma au vyama vya kisiasa.

“Maelezo yote tuliyoyatoa yanatosha kwa mtu yeyote mwenye nia ya kukagua sajili ya wapigakura. Hatuelewi maelezo zaidi ambayo ODM inahitaji. Iwapo tutatoa habari za kibinafsi za kila mpigakura, kazi ya ukaguzi wa sajili ya wapigakura inayofaa kufanywa na tume itakuwa hatarini,” wakasema mawakili wa IEBC, Edwin Mukele na Mahat Somane.

IEBC jana iliomba korti itoe uamuzi kuhusu siri ya maelezo ya raia na jukumu na haki za vyama vya kisiasa kushirikishwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi.

IEBC ilisema kwamba nambari za simu na ile ya kitambulisho ni habari ambazo hazifai kufichuliwa kwa chama cha kisiasa bila idhini ya mtu binafsi.

ODM kupitia mawakili wake James Orengo na Edwin Sifuna ilikuwa imeshikilia kwamba IEBC ilikuwa imekataa kuwapa habari muhimu kuhusu rejista ya wapigakura wa Kibra.

Uchaguzi huo mdogo utafanyika hapo kesho.

You can share this post!

Wahuni wa Sonko wapiga waandishi

Uhuru amcheka Maraga kuhusu masaibu kortini

adminleo