• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 4:10 PM
Wabunge wamtaka Matiang’i afute Kinoti, avunje Flying Squad

Wabunge wamtaka Matiang’i afute Kinoti, avunje Flying Squad

RICHARD MUNGUTI na CHARLES WASONGA

WABUNGE Jumanne wamemtaka Waziri wa Ulinzi Dkt Fred Matiang’i amsimamishe kazi Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi (DCI) George Kinoti, mkuu wa Kitengo cha Flying Squad Musa Yego, na kukifutilia mbali kwa madai kinatumiwa na watu wachache kuwatesa, kuwadhulumu kuwadunisha na kuwasumbua wafanya biashara na wawekezaji jijini Nairobi.

Licha ya kikosi hiku kutumiwa vibaya na wafanya biashara wachache, Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai “hajasema chochote na anahitajika kujibu maswali mengi sababu ya kuruhusu maafisa wa polisi wa Flying Squad kutumiwa vibaya

Wakiwahutubia wanahabari katika majengo ya Bunge, wabunge Babu Owino (Embakasi Mashariki) na George Sunkuiya (Kajiado magharibi) walitoa wito kwa Dkt Matiang’i atoe taarifa kuhusu vitendo vya maafisa hao wa Flying Squad.

Wawili hao walimsihi Dkt Matiang’i atoe taarifa kuhusu tabia ya maafisa hao wa Flying Squad pamoja na kuwasimamisha Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai George Kinoti na mkuu wa kitengo hicho Bw Musa Yego na maafisa wote waliomsumbua na kumkamata mmiliki na mstawishaji wa mtaa wa kifahari wa Kihingo Village (Waridi Gardens) ulioko Kitsuru, Bw James Ndung’u Gethenji.

Wabunge hao walisema katika taarifa yao kwamba licha ya Ndung’u kupiga ripoti kwa polisi hakuna hatua imechukuliwa.

“Inspekta Jenerali wa Polisi William Mutyambai amekuwa kimya licha kupokea ripoti hizi zote,” walisema Owino na Sunkuiya.

Wabunge hawa walilalamika kuwa baadhi ya wenye nyumba 17 katika mtaa huo wa Kihingo wameshirikiana na nduguye Ndung’u, Gitahi kumpokonya mtaa huo.

Na kwengineko mahakamani kesi dhidi ya walinzi wanne wa kampuni ya Classic Services inayotoa huduma katika makazi ya kifahari ya Kihingo Village (Waridi Gardens) eneo la Kitsuru walishtakiwa pamoja na mmiliki wa mtaa huo wenye thamani ya Sh20 bilioni unaomilikiwa na mbunge wa zamani wa Tetu James Ndung’u Gethenji.

Wamiliki wa mtaa huo Ndung’u na nduguye mkubwa Fredrick Gitahi Gethenji wamekuwa wakizozana kuhusu uthibiti na usimamizi wake.

Kutokana mtafaruku huu wa uthibiti na usimamizi wa mtaa huo kati unaowagonganisha ndugu hao polisi wa kitengo cha Flying Squad kilichoko chini ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) wamemtia nguvuni Ndung’u mara mbili na kumfikisha kortini.

Ndung’u, alitiwa nguvuni Julai 2 2019 na kufikishwa mbele ya hakimu mkuu Martha Mutuku na kushtakiwa pamoja na mkurugenzi mwenza wa Kihingo Village (Waridi Gardens) Limited ,Chacha Mabanga na Frankline Mutegi.

Walinzi walioshtakiwa pamoja na watatu hao ni Josiah Augo Otimo, Geoffrey Ochieng Okello, Kennedy Ochieng Asewe na Shadrack Ouma Okonji.

Wote sasa wanakabiliwa na shtaka la kuvuruga amani, kujeruhiwa , kuzua vurugu na kuharibu mali.

Kujumulishwa kwao kumetimisha saba washukiwa wanaokabiliwa na mashtaka ya kutoa fujo mtaani Kihingo Village mnamo Julai 2, 2019.

Wote saba walifika mbele ya hakimu mkuu Martha Mutuku ambaye aliamuru kesi hiyo isikizwe Novemba 18, 2019.

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Matumizi sahihi ya vivumishi vya pekee hasa...

Takwimu za sensa ni feki sana – Magavana

adminleo