• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Timizeni ahadi zenu, balozi wa Amerika arai wanasiasa

Timizeni ahadi zenu, balozi wa Amerika arai wanasiasa

Na PIUS MAUNDU

BALOZI wa Amerika nchini Kenya, Bw Kyle McCarter amewashauri wanasiasa wanaotarajia kuchaguliwa tena mamlakani mwaka wa 2022 waharakishe kutekeleza ahadi walizotolea wananchi.

Seneta huyo wa zamani wa Illinois alisema utekelezaji wa ahadi zinazotolewa uchaguzini huwapa wanasiasa nafasi bora ya kuchaguliwa tena.

“Si vigumu kutimiza mahitaji yanayomfanya kiongozi afanikiwe. Fanya yale uliyosema utafanyia wananchi wakati wa kampeni,’ akasema alipozuru Kaunti ya Makueni wikendi.

Bw McCarter alisema hatua hii hufanya wananchi kuwaenzi viongozi na hivyo kupunguza gharama za kufanya kampeni.’Unapotenda yale uliyosema utatenda, wananchi watakubali wewe ni kiongozi bora.

Walio na sifa ya kutenda mema na kutimiza ahadi zao huwa hawatumii fedha nyingi katika kampeni zao,’ akasema.

Balozi huyo alizuru baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Amerika kupitia kwa mashirika yake mbalimbali yaliyo nchini.

Kwanza alijumuika na Gavana wa Makueni, Prof Kivutha Kibwana kuzindua Sera ya Maji ya Kaunti ya Makueni.Sera hiyo inatoa mwongozo wa mipango na ustawishaji wa usimamizi wa rasilimali za maji katika kaunti hiyo.

Baadaye wawili hao walisimamia ‘mahafali’ ya watoto ambao hawajaambukizwa HIV licha ya kuwa hatarini kwa miezi 18, kwani waliekwa chini ya mpango wa kuzuia maambukizi kutoka kwa mama hadi mtoto. Mpango huo unafadhiliwa na Amerika.

Walitembelea pia Hospitali ya Makueni Mother and Child iliyo na ukubwa wa kulaza wagonjwa 200 mjini Wote.

Hospitali hiyo ilijengwa na kununuliwa vifaa kwa gharama ya Sh135 milioni na serikali ya kaunti.Baada ya hapo, walizindua mradi wa maji wa Makutano katika eneo la Kathonzweni.

You can share this post!

Polisi wageuka wanyama ghafla wakizima maandamano JKUAT

Wazee wa Agikuyu sasa wapanga kusimamia tohara

adminleo