• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Bwanyenye Kariuki aruhusiwa kusafiri majuu

Bwanyenye Kariuki aruhusiwa kusafiri majuu

Na RICHARD MUNGUTI

MMILIKI wa kampuni ya kutengeneza pombe ya Africa Spirits Limited (ASL) Humphrey Kariuki anayekabiliwa na shtaka la kukwepa kulipa ushuru wa Sh41 bilioni  ameruhusiwa kusafiri ng’ambo kushughulikia biashara zake kwa siku 15.

Akiruhusiwa kusafiri, Bw Kariuki aliamriwa na hakimu mkuu mahakama ya Milimani Francis Andayi arudishe pasipoti zake mbili kortini mnamo Desemba 6, 2019.

Mbali na kukubaliwa kusafiri, Karikuki aliagizwa awasilishe mahakamani orodha ya nchi atakazozuru.

“Nakuagiza uwasilishe mahakamani orodha ya nchi utakazozuru kuwezesha mahakama kujua kule uliko,” alisema Bw Andayi.

Ombi la kusafiri ng’ambo liliwasilishwa na wakili Cecil Miller aliyemweleza mahakama mshtakiwa aliyekana kesi tatu dhidi yake pamoja na washtakiwa wengine wanane “hana budi kurudi kwa vile amewekeza mali mengi nchini.”

Kariuki aliachiliwa kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh11 milioni.

You can share this post!

Niliipata maiti ya Monica kwa bafu, shahidi asimulia...

StandChart yaagizwa itoe ushahidi katika wizi wa Sh827m

adminleo