• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
Mwili wa polisi aliyetoweka wapatikana ukining’inia mtini

Mwili wa polisi aliyetoweka wapatikana ukining’inia mtini

Na JACOB WALTER

MWILI uliokuwa umeanza kuoza wa afisa wa polisi aliyetoweka mnamo Novemba 18, 2019, ulipatikana Ijumaa ukining’inia mtini huko Araftiris eneo la Sabare, Horr Kaskazini kaunti ya Marsabit.

Kulingana na Kamanda wa Polisi eneo la Horr Kaskazini, Mohammed Abdigaran, wafugaji waliripoti katika kituo cha polisi cha Dukana kwamba waliona mwili ulioshukiwa kuwa wa afisa wa polisi ukining’inia mtini kwenye barabara ya Buluk eneo la Araftiris.

“Tulipata ripoti kutoka kwa mzee wa jamii ya Gabbra kuhusu mwili ulioonekana ukining’inia mtini eneo la Buluk katika kijiji cha Sabare. Mtu huyo aliyefariki alitambuliwa mara moja kama Konstebo Abdiaziz Mohammed Aden, afisa kutoka kituo chetu cha polisi,” alisema Bw Abdigaran.

Mzee Bw Guyo Tete, alipiga ripoti katika kituo cha polisi mnamo Novemba 21, 2019 mwendo wa saa nne kasoro dakika tano asubuhi.

Maafisa wa polisi waliweza kumtambua marehemu kama konstebo wa polisi kutoka kitengo cha kulinda mpaka eneo la Dukana.

Mwili huo ulipatikana ukiwa umefungwa mtini kwa kamba huku mkoba na nguo zilizoshukiwa kuwa za mwendazake zikiwa zimetawanyika mita chache kutoka eneo hilo.Alisema mipango ya kusafirisha mwili kutoka eneo hilo hadi Horr Kaskazini na hatimaye mjini Marsabit ilitatizwa na hali mbaya ya anga.

You can share this post!

Yafichuka wafanyakazi wa serikali wanafilisisha nchi

DINI: Ufalme wa mbinguni ni kama karamu ya harusi,...

adminleo