• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:30 PM
Kilio KDF wanatesa wakazi Tana River

Kilio KDF wanatesa wakazi Tana River

NA STEPHEN ODUOR

VIONGOZI wa kidini katika eneo bunge la Garsen, kaunti ya Tana River wamelalamika kwamba wanateswa na wanajeshi wa Kenya (KDF).

Wakisimulia masaibu yao kwa Taifa Leo, viongozi hao wa kidini walisema kwa muda sasa, wamekuwa wakikamatwa kiholela na kupigwa bila sababu na baadaye kuachiliwa.

‘Walitukamata tukiwa tumetoka kwa hafla ya wazi mjini Garsen kuelekea msikitini wakasema sisi ni washukiwa wa ugaidi,’ alielezea Ustadh Hussein Abdi.

Maafisa hao baadaye waliwapeleka zaidi ya kilomita ishirini msituni wakiwa wamewafunga macho,ambapo waliwapiga kwa siku tatu mfululizo.

Walimu hao watatu wa dini walieleza kuwa kwa siku tatu, waliamshwa kwa fimbo na kumwagiwa maji usoni,huku wakilazimishwa kula nyama mbichi.

You can share this post!

Wazee wa Pwani wakataa BBI

DINI: Ukitaka kufanikiwa katika hatua zako maishani, lazima...

adminleo