• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
BBI: Ruto abuni mikakati ya kuzima Uhuru na Raila

BBI: Ruto abuni mikakati ya kuzima Uhuru na Raila

Na WAANDISHI WETU

NAIBU Rais William Ruto ameweka mikakati ya kuwalemea Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika juhudi za kudhibiti mjadala kuhusu ripoti ya Jopo la Maridhiano (BBI).

Mojawapo ya mikakati hiyo ni kubadili msimamo kuhusu kura ya maamuzi, kuundwa kwa miungano ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ambao watatangaza ajenda yake mashinani kuanzia wiki ijayo na kushirikisha mawaziri na uongozi wa bunge, kupitia Spika wa Seneti Ken Lusaka, katika mipango hiyo.

Dkt Ruto na wandani wake pia wameamua kubadili mkakati wao wa kisiasa kwa kuweka kando msimamo wao wa awali kuwa ripoti hiyo ishughulikiwe na bunge pekee.

Sasa wamekumbatia kura ya maamuzi kama mojawapo ya njia za kushughulikia baadhi ya mapendekezo ya ripoti hiyo ya BBI iliyozinduliwa mwezi jana.

Kwanza wafuasi wa Naibu Rais tayari wameunda miungano miwili ya viongozi; muungano mmoja unaoshirikisha wandani wake kutoka Mlima Kenya na pili muungano wa washirika wake kutoka Rift Valley.

Muungano wa Mlima Kenya unaongozwa na Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri na uliandaa mkutano wake wa kwanza mjini Embu wiki jana. Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na zaidi ya wabunge 40 kutoka eneo hilo uliafikia kuwafundisha wananchi kuhusu ripoti ya BBI katika eneo hilo.

Mungano wa Rift Valley nao unaongozwa na Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri na kufanya mkutano wake wa kwanza mjini Naivasha Alhamisi na Ijumaa kupanga mikakati ya kuendeleza ajenda hiyo hiyo ya kunadi ripoti ya BBI katika eneo hilo.

Makundi hayo mawili ya wafuasi wa Dkt Ruto yametangaza kuwa yako tayari kuunga mkono utekelezaji wa ripoti ya BBI kupitia mkondo wa Bunge na Kura ya Maamuzi.

“Tumewasikia wengine wakidai kuwa bunge haliwezi kuaminiwa kuunda sheria,” wabunge wa Rift Valley wakasema.

You can share this post!

Muungano wa Ruto na Kalonzo wang’oa nanga

JAMVI: Hakuna dalili za NASA kujifufua tena kwa ajili ya...

adminleo