• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 7:50 AM
Nishati ya jua kusaidia kuimarisha uzalishaji wa maua Thika

Nishati ya jua kusaidia kuimarisha uzalishaji wa maua Thika

NA LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya maua ya Simbi Roses Ltd eneo la Thika, kaunti ya Kiambu, imeweka mtambo mpya wa nishati ya jua utakaoongeza nguvu zaidi za utendaji kazi.

Mtambo huo wa kipekee umeundwa kwa paneli 454 za nishati ya jua nguvu  na utahifadhi tani 144 za gesi ya CO2 kwa mwaka moja.

Mtambo huo unao uwezo wa kupunguza gesi aina ya C02 kwa na utumizi mwingi wa umeme.

Kulingana na kampuni hiyo, mtambo huo una uwezo wa kutoa umeme wa kutosha wakati wa mchana.

Kampuni hiyo hivi majuzi imefanya ushirikiano wa karibu na kampuni ya Ecoligo ya Ujerunani iliyo na tawi lake hapa nchini Kenya. Wakati huo pia inaendesha shughuli zake chini ya mwavuli wa Germany Energy Solution Initiative.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Simbi Roses Bi Grace Nyachae, alipongeza ushirikiano mzuri uliopo wa kampuni ya Ecoligo na Project Development Programme (PDP)..

“Kutokana na mpango huu mpya kampuni ya Simbi Roses itapunguza utoaji wa gesi ya C02 na utumizi wa umeme kwa kiwango cha juu na kuipa kampuni nafasi ya kuendesha kazi yake kwa njia ifaayo,” alisema Bi Nyachae.

Alisema kampuni hiyo inaendelea kupata maua za hali ya juu kulingana na hali nzuri ya hewa na jinsi wanavyonyunyizia maji.

Alisema kutokana na kazi yao ya kutamanika, wanaweza kupanda na kusafirisha nje aina 13 tofauti za maua.

Baadhi ya maua hayo ni Bellerosa, Red Ribbon, Good Times, Sona Risa, vanilla Sky, Marie Claire, Mario, High & Magic na Upper Class.

 

You can share this post!

Kizimbani kwa kuuma polisi sikio kisha kumzaba kofi

Mzee wa kanisa mpenda uroda afichuliwa

adminleo