• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 10:06 AM
Juhudi za kuzima ‘muguka’ zafeli

Juhudi za kuzima ‘muguka’ zafeli

Na Farhiya Hussein

KAUNTI ya Mombasa haijafanikiwa kuangamiza utafunaji Muguka, kwani biashara hiyo bado ni maaarufu eneo la Pwani.

Hapo mbeleni, maafisa wa kaunti walivunja zaidi ya vibanda 100 vinavyouza Muguka ili kumaliza janga hilo la utumizi wa Muguka lakini bado nguvu zao hazikufua dafu kwani bado soko la Muguka linapanuka katika kaunti hiyo.

“Baadhi yetu tunapata pesa za kujilisha na kulisha watoto wetu kwa hili biashara. Hakuna anayelazimishwa kununua Muguka, haya ni mateso bure,” akalalamika Joe Mramba muuzaji mmoja.

Akizungumza na Taifa Leo, naibu mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la kaunti, Bi Fatuma Kushe alisema suala la Muguka limewasilishwa katika kikao cha bunge na wakatoa maamuzi ya kupiga marufuku.

“Tunataka kuongoza vyema. Si kupiga marufuku kisha yaishie hapo. Tuwekeze mikakati kwanza itakayofuatiliwa kuhakikisha uuzaji wa Muguka haurudi sokoni,” alisema Bi Kushe.

You can share this post!

Maimamu wataka tume mpya ibuniwe kusaidia EACC

Sakaja sasa amezea mate kiti cha Sonko

adminleo