• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
KCSE 2019: Kenya High yapepea

KCSE 2019: Kenya High yapepea

Na WANDERI KAMAU

SHULE ya Upili ya Kenya High ilitoa idadi kubwa ya wanafunzi waliopata alama ya ‘A’ kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE) yaliyotangazwa Jumatano.

Wanafunzi 76 walipata alama ya ‘A’ katika shule hiyo, ikilinganishwa na wanafunzi 11 pekee waliopata alama hiyo mnamo 2018.

Shule hiyo iliishinda Shule ya Upili ya Alliance, ambayo ndiyo iliongoza nchini mwaka uliopita wanafunzi 35 wakizoa alama ya ‘A’. Na licha ya kutoibuka bora, idadi ya ‘A’ shuleni humo iliongezeka kutoka 35 hadi 48 mwaka huu.

Shule ya Upili ya Wavulana ya Kapsabet iliyo katika Kaunti ya Nandi iliibuka ya pili wanafunzi 49 wakipata ‘A’. Hii ni ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo wanafunzi 26 ndiyo walizoa alama hiyo.

Maseno School ilipata ‘A’ 23 mwaka huu, ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo wanafunzi 10 pekee ndio walipata alama hjyo.

Shule ya Upili ya Mang’u pia iliongeza idadi yake ya ‘A’ kutoka 16 mwaka uliopita hadi 23 mwaka huu.

Hali ilikuwa hivyo kwa Shule ya Moi High School Kabarak ambayo iliongeza idadi hiyo kutoka 28 hadi 30 mwaka huu nayo Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi Eldoret ikiongeza idadi hiyo kutoka 13 hadi 21.

Shule zingine 10 bora zilizopata alama nyingi za ‘A’ mwaka huu ni Alliance Girls ambapo wanafunzi 27 walipata alama hiyo kutoka 21 mwaka uliopita, Mary Hill Girls (25) na Nairobi School (23).

Akitoa matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Prof George Magoha alisema kuwa kwa jumla, idadi ya wanafunzi waliopata ‘A’ mwaka huu iliongezeka kutoka 315 mnamo 2018 hadi 627.

Waziri alisema kuwa hali hiyo imechangiwa na mikakati thabiti ambayo wizara yake imeweka kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kukabili visa vya udanganyifu kwenye mitihani.

You can share this post!

Wizi wapungua KCSE 2019

KCSE 2019: Wasichana waendelea kuandikisha matokeo bora

adminleo