• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
KRISMASI: Ni wakati wa kupunguza siasa, viongozi waambiwa

KRISMASI: Ni wakati wa kupunguza siasa, viongozi waambiwa

Na Macharia Mwangi

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Mombasa Martin Kivuva ametoa wito kwa viongozi wasitishe siasa ili kuwapa Wakenya wakati mwafaka wa kusherehekea Krismasi.

Askofu Kivuva alisema huu ni wakati wa kuhubiri amani, upendo na umoja na pia Wakenya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo na kushiriki matendo yanayonufaisha jamii.

Aidha, alitoa wito kwa viongozi kuweka kando tofauti zao za kisiasa wakati huu wa Krismasi na kuungana pamoja kuhubiri amani miongoni mwa Wakenya wote.

“Huu ni wakati wa kunyenyekea na kuungana kusherehekea upendo wa Kristo. Naomba tuweke siasa kando ili Wakenya waungane kusheherekea Krismasi kwa upendo,” akasema.

Vilevile aliwaomba Wakenya kuombea familia zao na wasiobahatika katika jamii na pia kuwakumbuka katika sherehe zao.

“Ni vyema kushiriki matendo ya kibinadamu kwa kuwatembelea wagonjwa na kula pamoja na wanaokosa mlo. Kwa ujumla huu ni wakati wa kutenda mema,” akaongeza.

 

You can share this post!

Vigogo wa kisiasa wanavyomumunya Krismasi

Jaji Odek alifariki kwa damu kuganda mguuni – Serikali

adminleo