• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 1:51 PM
Nafasi za kazi kwa wanaosaka ajira

Nafasi za kazi kwa wanaosaka ajira

NA MARY WANGARI

Nini: Mwalimu Mkuu, Walimu wa Grade 1, PP1

Wapi: Shule ya The Firm Roots

Unachohitaji:

Cheti cha digrii au stashahada

Nambari ya Usajili ya TSC

Tuma nakala za vyeti na tawasifu yako kupitia: [email protected] kabla ya Januari 30.

 

Nini: Wahudumu, Wapishi, Wahasibu

Wapi: Bonds Garden

Tuma nakala ya tawasifu yako kupitia [email protected]

Nini: Mhudumu Mwanamke

Wapi: Super Metro

Majukumu:

Kuwasalimia abiria wanapoabiri

Kujibu maswali ya abiria

Kuelekeza abiria kwa viti wanavyotaka

Wajibu:

Sharti uwe mwanamke mwenye umri kati ya 22 na 27

Uwe na stashahada katika Elimu

Uwezo kwa kuwasiliana kwa Kiingereza na Kiswahili

Ikiwa ungependa kazi hii, dondosha nakala ya barua yako ya maombi katika afisi za Super Metro.

 

Nini: Msimamizi wa Vyakula Hotelini

Wapi: Nairobi

Unachohitaji:

Stashahada katika Huduma ya Hoteli

Ufahamu kuhusu maakuli anuai

Endapo umevutiwa na kazi hii, tuma maombi kupitia, [email protected]

 

Nini: Mwalimu wa ECD

Wapi: Kidogo Innovations

Ikiwa unapenda kufanya kazi na wamiliki vituo vya kulelea watoto, basi shirika hili linakutafuta.

Unachohitaji:

Stashahada katika ECD

Ikiwa ungependa kazi hii, tuma maombi kupitia: [email protected] au upige simu kupitia 0731239757 kwa maelezo zaidi.

 

Nini: Wauzaji bidhaa

Wapi: Nakuru, Nairobi

Ikiwa ungependa kazi hii, tuma nakala ya tawasifu yako kupitia: [email protected], Cc [email protected]

 

Nini: Walimu: Hissabati/Fizikia, Kiingereza/Fasihi, Mziki, Sanaa na Mitindo

Wapi: Shule ya Upili ya Wasichana ya Ukwala

Ikiwa ungependa kazi hii wasiliana nao kupitia 0721206912. Tuma nakala ya barua ya kuomba kazi kupitia: [email protected]

 

Nini: Maafisa wasaidizi

Wapi: Kaunti ya Taita Taveta

Unachohitaji:

Cheti cha KCPE

Tuma nakala za maombi yako kwa:

Katibu, Bodi ya Kaunti kuhusu Utowaji Huduma Private Bag Voi au udondoshe katika afisi za bodi.

 

Nini: Walimu

Wapi: Shule ya Upili ya Wasichana ya Consolata

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nao kupitia: 0712418035, 0731185577

 

Nini: Mwalimu wa ECD

Wapi: Mradi wa Kitendo kuhusu Ufadhili kwa Watoto, Naivasha

Unachohitaji:

Digrii katika BA/BSc au tajriba ya HND

Uwe na stashahada au cheti cha ualimu

Uwe umesajiliwa na TSC

Endapo ungependa kazi hii tuma tawasifu pamoja na barua ya kuomba kazi kupitia [email protected]

 

Nini: Afisa wa mauzo kidijitali

Wapi: Glantix Solutions, Nairobi

Unachohitaji:

Stashahada au Digrii katika Teknohama au nyanja za mauzo

Ujuzi wa mauzo kidijitali

Umakinifu wa kiwango cha juu

Ikiwa umevutiwa na kazi hii tuma nakala za barua ya kuomba kazi na tawasifu yako kupitia [email protected]

 

Nini: Dereva

Wapi: Kampuni ya Norbrook, Limuru

Unachohitaji:

Cheti cha KCSE

Ujuzi kuhusu kanuni za kiviwanda

Leseni halali ya kuendesha gari daraja BCE

Tuma barua kupitia baruameme:human.resources@norbrook.co.uk

 

Nini: Mhudumu wa kuuza vileo

Wapi: Hoteli ya Urban Point, Parklands, Nairobi

Majukumu:

Kuwasalimu na kuwasindikiza wateja mezani pao

Kuwasilisha orodha ya vinywaji au vyakula na kutoa ufafanuzi unapoagizwa

Kuandaa meza kwa kutandika vitambaa, kupanga bilauri na vyombo vinginevyo

Tuma tawasifu yako ukinukuu jina Mhudumu kwenye anwani kupitia baruameme: [email protected]

 

Nini: Maafisa wa kuzima moto (35)

Wapi: Mamlaka ya Usafiri wa Ndege Nchini (KAA)

Majukumu:

Kutoa huduma za kuzima moto na uokoaji katika ajali za ndege na majengo yanayoteketea

Kukagua magari, mitambo na vifaa kuhakikisha viko shwari

Kukagua mikondo na barabara zinazopitiwa na ndege na teksi

Unachohitaji:

Cheti cha KCSE kuanzia alama C

Uwe mzima kiafya Cheti cha Nidhamu

Tuma nakala za vyeti vyako pamoja na tawasifu kupitia [email protected] au kupitia barua kwenye anwani:

[email protected]

Usikubali mtu yeyote kukuitisha hela ili akupe ajira. Taifa Leo Dijitali haitawajibikia matukio ya ulaghai kutokana na nafasi za kazi tunazochapisha.

You can share this post!

Hofu Marekani ikipunguza ufadhili nchini

Polisi wazima mkutano wa Mudavadi Mumias

adminleo