• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 8:50 AM
Ipoa yachunguza matukio ya maafisa kuwafyatulia risasi wanaume wawili

Ipoa yachunguza matukio ya maafisa kuwafyatulia risasi wanaume wawili

Na PETER CHANGTOEK

MAMLAKA Huru ya Kuwapiga Msasa Polisi (Ipoa) imeanzisha uchunguzi wa matukio ambapo maafisa waliwafyatulia risasi wanaume wawili katika mitaa ya Majengo na Mwiki, Nairobi, amesema Mwenyekiti Bi Anne Makori.

Katika tukio la mtaani Majengo, polisi inadaiwa ‘walilazimika’ kutumia vitoa machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wakizua fujo baada ya mmoja wao kupigwa risasi na polisi, katika mtaa wa Majengo, Nairobi akishukiwa kuwa mwizi.

Maafisa hao walikuwa na hali ngumu kuwatuliza vijana hao ambao walikuwa wakiwakabili kwa kuwarushia mawe, huku wakiwasha tairi katika barabara ya Meru Road, mtaani huko.

Vijana hao walilalamikia kupigwa risasi kwa mwenzio, ambaye walidai aliuawa bila hatia katika mtaa huo, mnamo siku ya Alhamisi mchana.

“Ahmed hakuwa mwizi, amekuwa akiwafunza vijana kutumia viatu vya magurudumu; skating,” alisema mmoja kati ya vijana hao.

Hata hivyo, madai hayo hayakuthibitishwa na gazeti hili, kwa kuwa hatukumpata afisa mkuu wa polisi ili atoa maonikuhusiana na tukio hilo.

Biashara katika mtaa huo zililazimika kufungwa kwa muda wa takribani saa mbili wakati makabiliano hayo yalikuwa yakiendelea baina ya maafisa wa polisi na waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu.

Shughuli za usafiri, vilevile, ziliathirika maadamu barabara hiyo inayoelekea Gikomba, ilikuwa imefungwa, huku moto ukiwashwa barabarani.

Hata hivyo, hakuna yeyote aliyekamatwa wakati wa purukushani hiyo.

You can share this post!

DAU LA MAISHA: Kajenga himaya ya biashara mtandaoni

Polisi watumia vitoa machozi kutibua mkutano wa Mumias

adminleo