Babayao ataka ushahidi mkuu ung'olewe
Na RICHARD MUNGUTI
MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) ameomba mahakama itupilie mbali ombi la aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ushahidi muhimu katika kesi ya ufisadi inayomkabili ya Sh580 milioni ukataliwe.
Bw Waititu amepinga kufika kortini kwa afisa mkuu wa masuala ya fedha Kaunti ya Kiambu Bw Justus Bundi Kinoti na Mkurugenzi wa masuala ya uagizaji bidhaa na huduma Bi Faith Njeri Harisson kutoa ushahidi dhidi yake.
Bw Waititu anadai Njeri na Bundi walikuwa miongoni mwa maafisa wakuu katika Kaunti ya Kiambu walioidhinisha malipo hayo ya Sh580 milioni.
“Njeri na Bundi ni miongoni mwa maafisa walioshiriki kutoa maamuzi yaliyopelekea pesa zilipwe mwanakandarasi aliyeteuliwa kukarambati barabara katika kaunti hiyo,” wakili John Swaka anayemwakilisha Bw Waititu amemweleza hakimu mwandamizi Thomas Nzioki.
Akiomba korti itupilia mbali ombi hilo la Bw Waititu, kiongozi wa mashtaka Bw Nicholas Mutuku, alisema Bw Waititu anataka kuchelewesha kusikizwa kwa kesi ya ufisadi inayomkabili.
Bw Mutuku amesema hatua hii ya Bw Waititu “ni tisho kuu kwa mashahidi walioorodheshwa.”
Kiongozi huyo wa mashtaka ameambia mahakama Bw Waititu hajasema ataathiriwa aje na mashahidi hao wakitoa ushahidi dhidi yake.
Bw Mutuku amesema DPP ameruhusiwa kisheria kuita idadi ya mashahidi anaowataka pasi na ubaguzi.
“Sio jukumu la Bw Waititu ama mshtakiwa mwingine yeyote kuchagua mashahidi watakaotoa ushahidi,” alisema Bw Muteti.
Na wakati huo huo Bw Waititu aliwasilisha ombi katika mahakama kuu kupinga uamuzi wa Seneti wa kumtimua uongozini kwa madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.
Hata hivyo kesi hiyo haikukubaliwa na idara ya usajili wa idara ya mahakama.
Mawakili hao walishauriwa wakarekebishe
Naibu wa DPP Nicholas Mutuku alimweleza hakimu mwandamizi Thomas Nzioki , jaribio hilo la Bw Waititu kwamba gavana Waititu hana uwezo wa kumchagulia DPP mashahidi atakaowaita kutoa ushahidi.
Mahakama iliomba ikatae ombi hilo la mshtakiwa na kuruhusu kesi iendelee.