Sekta za elimu na afya kufaidi pakubwa kwa bajeti ya ziada

Na CHARLES WASONGA
SEKTA za elimu na afya ndizo zitafaidi pakubwa katika bajeti ya ziada ya kima cha Sh40 bilioni iliyowasilishwa bungeni Jumatano.
Kwenye makadirio hayo yaliyowasilishwa na kiongozi wa wengi Aden Duale, walimu, wahadhiri, madaktari, wauguzi na wahudumu wengine wa afya wametengeza fedha za kutekeleza nyongeza za mishahara na marupurupu zao.
Huenda hatua hiyo ikapeleleza wafanyakazi hao, haswa wahadhiri kufutilia mbali mgomo wao ambao sasa umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na kuvuruga shughuli za masomo katika vyuo 33 vikuu vya umma.
Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) imetengewa Sh16 bilioni ambazo zinatarajiwa kutumika kuajiri walimu 68,000 wa vibarua kukabiliana na kero la uhaba wa walimu katika shule za umma.
Aidha, TSC ilikuwa imeiomba itengewe Sh5 bilini ili iweze kuajiri walimu 12,696 zaidi kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne ili kufanikisha mpango wa serikali wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanaofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) wanajiunga na shule za upili.
Idara ya Elimu ya Vyuo Vikuu pia imetengewa Sh5.7 bilioni ambazo zitatumika kugharamia makubaliano kuhusu nyongeza ya mishahara (CBA) kati ya serikali na wahadhiri hatua ambayo inatarajiwa kuzima mgomo wa unaoendelea sasa.
Wahadhiri hao wamekuwa wakitaka serikali iwalipe kitita cha Sh38 bilioni kwa CBA yao ya 2017 hadi 2021, lakini vyuo vikuu viliamua kuwalipa Sh6.8 bilioni lakini kwa idhini ya serikali.
Idara ya elimu ya msingi imetengewa Sh1.9 bilioni ambazo zitatumika kuligharamia malipo ya marurupu ya walimu. Idara hiyo pia imetengewa Sh2.6 bilioni za kufadhili miradi ya maendeleo.

“Hata hivyo, Sh7.2 bilioni zimeondolewa kutoka bajeti ya Vyuo vikuu ambayo ilikusudiwa kutumika kufadhili miradi ya maendeleo.

Habari zinazohusiana na hii

KENYA IMESOTA!