• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Mwanamke aliyejeruhi wanawe kwa kisu ana akili timamu – ripoti

Mwanamke aliyejeruhi wanawe kwa kisu ana akili timamu – ripoti

NA BRENDA AWUOR

MWANAMKE aliyedunga watoto wake wanne kwa kisu cha nyumbani ataendelea kuzuiliwa Kodiaga, baada ya ripoti kutoka hospitalini kuonyesha kuwa ana akili timamu.

Ripoti kutoka hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH) imeonyesha kuwa, Mercy Anyango, 29, mkazi wa eneo la Awasi, Kisumu, aliyepatikana na hatia ya kudunga watoto wake wanne kisha kujidunga hana kasoro yoyote kiakili.

Mshtakiwa, alipimwa akili katika hospitali ya JOORTH, baada ya mahakama ya Nyando kutoa amri kuwa apimwe akili jinsi alivyoomba kiongozi wa mashtaka Bi Maureen Odumba, mnamo Januari 24, 2020, kesi ilipokuwa ikitajwa.

Ripoti ya matokeo ilipoonyesha kuwa hana kasoro, korti ilitoa amri kuwa azuiliwe katika gereza la Kodiaga, uchunguzi mwingine ukifanywa hasa kuhusu kile ambacho kilimsukuma kuwadunga wanawe kwa kisu mara kadhaa.

Bi Anyango aliyeshtakiwa kwa kosa la kudunga watoto wake wanne mnano Januari 7, mbele ya hakimu mkazi mkuu Reuben Sang, alikubali mashtaka yote matano huku akiomba korti ya Nyando imsamehe na kumpa fursa ya kulinda wanawe.

Alisomewa mashtaka ya kuwadunga watoto wake na kusababisha majeraha mengi kwao, na alikubali mashtaka na kuomba msamaha.

“Naomba korti inisamehe kwani niliyoyafanya ni sababu ya hasira baada ya mume kuniacha na majukumu. Bado nawapenda wanangu,’’ aliomba.

Mshtakiwa pia alikubali kosa la kutaka kujiua, kwa kujidunga shingo na tumbo kwa kutumia kisu kilekile baada ya kudunga wanawe kinyume cha sheria.

Baada ya kudunga wanawe na kusababisha majeraha kwao ,ripoti ilisema kuwa, majirani walisaidia waathirika baada ya kusikia vilio na kisha kupiga ripoti kwa kituo cha polisi, Awasi.

Waathirika wote waliwahiwa katika hospitali ya JOOTRH ambapo hadi sasa, wanaendelea kupokea matibabu.

You can share this post!

Dkt Ruto ashauri maombolezo na mazishi ya Moi yasiingizwe...

Wanafunzi kutoka Kenya walio China wasema serikali...

adminleo