• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 12:48 PM
Walimu wapinga ajira ya kandarasi

Walimu wapinga ajira ya kandarasi

Na RICHARD MUNGUTI

WALIMU waliohitimu na ambao hawajaajiriwa na tume ya walimu nchini TSC wamepinga hatua ya kuajiriwa kama vibarua.

Katika kesi iliyoratibishwa kuwa ya dharura na Jaji Hellen Wasilwa walimu hao wanateta kuwa TSC inakandamiza haki zao za kuajiriwa kwa mujibu wa sheria badala kuwapa kazi ya kibarua.

Jaji Wasilwa aliombwa asitishe ajira ya walimu vibarua 10,300 hadi kesi iliyoshtakiwa na Bw Lempaa Suyianka isikizwe na kuamuliwa.

“Katika tangazo iliyochapishwa katika mojawapo ya Magazeti watakaofaulu kupewa kazi hiyo ya kibarua lazima wawe wamejilipia Bima,” Jaji Wasilwa alielezwa.

Jaji huyo alifahamishwa kuwa sharti jingine ni kwamba watakaofaulu wawe tayari kupelekwa mahala popote pale kufanyakazi yao.

Mahakama ilielezwa TSC haizingatii haki za walimu hawa ikitiliwa maanani mahala kwingine humu nchini hakuna usalama wakutosha.

Jaji Hellen Wasilwa. Picha/RICHARD MUNGUTI

“Walimu wanahofia maisha yao ikitiliwa maanani TSC haitaki kuwaajiri walimu na kuwalipia bima,” Jaji Wasilwa alielezwa.

Mahakama ilielezwa haki za kimsingi za kila mfanyakazi lazima sizingatiwe na kuomba korti iratibishe kesi hiyo kuwa ya dharura.

Mlalamishi ameshtaki TSC, Tume ya Uuwiano wa Mishahara ya watumishi wa Umma (SRC) na mwanasheria mkuu.

Mahakama ilielezwa TSC iliandikiwa barua ifafanue jinsi ilivyofikia uamuzi kwamba Walimu waliohitimu kusomesha shule za msingi watakuwa wanaopokea Sh10,000.

Pia TSC iliombwa ifafanue jinsi walimu waliohitimu kusomesha shule za upili watakuwa wanapokea ajira ya Sh15,000.

“TSC haikufafanua utaratibu iliyofuata kupima kiwango cha ajira ambacho walimu wangelipokea cha Sh10,000 (walimu wa shule za msingi) na Sh15,000 (walimu wa sekondari),” Jaji Wasilwa alifahamishwa.

Barua sawa na hiyo iliyopelekewa TSC kuhusu malipo hayo ilipelekwa kwa SRC na vile vile hakukuwa na majibu.

Mahakama ilifahamishwa barua hizo zilipelekwa kwa tume hizo Desemba 2 2019 na kufikia sasa hazijajibiwa.

Katika tangazo iliyochapishwa na TSC , walimu 4,300 watapewa kazi ya vibarua na kupelekwa katika shule za msingi.

Walimu wapatao 6,000 watapelekwa shule za upili.

TSC iliwataka watakaohitimu wawe wamejiandikisha nalo na kupewa nambari za kusubiri kuajiriwa.

Mahakama ilielezwa TSC iliwafahamisha walimu hao kuwa watafanyakazi ya kibarua kwa muda wa miezi 12 na “ hakuna uhakika wataajiriwa siku za usoni.”

Jaji Wasilwa aliamuru nakala za kesi zipelekewe washtakiwa (tsc, src na ag) kisha isikizwe Feburuari 24, 2020.

You can share this post!

Tumaini, Isiolo Starlets zavuna Chapa Dimba

Prof Ojienda aendelee kuchunguzwa – Mahakama

adminleo