• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Wataalamu wataka mapendekezo muhimu yazingatiwe kulainisha utoaji mikopo

Wataalamu wataka mapendekezo muhimu yazingatiwe kulainisha utoaji mikopo

Na MAGDALENE WANJA

WATAALAMU wa sekta ya fedha wametaka kutekelezwa kwa mapendekezo katika mikopo ili kuweka uwazi na kupunguza idadi ya riba inayotozwa na wanaotoa mikopo.

Wataalamu hao wamesema kuwa mapedekezo hayo ni pamoja na mifumo ya utoaji wa taarifa ya mikopo, miundo ya kisheria, na usajili wa dhamana.

Washikadau hao wanahudhuria kongamano la tano la Africa Credit Information Sharing (CIS) jijini Nairobi.

Mkurugenzi mkuu wa CIS Bw Mr Jared Gatenga alisema kuwa kumekuwa na changamoto ambazo ni pamoja na kiwango cha juu cha riba.

“Ni muhimu kuwa na miundombinu ya mkopo ambayo itawawezesha watu kupata mikopo ambayo ni salama,” alisema Bw Gatenga.

Washikadau na wataalamu wa sekta ya fedha wanaohudhuria kongamano la tano la Africa Credit Information Sharing (CIS) jijini Nairobi. Picha/ Magdalene Wanja

Mwenyekiti wa CIS Bw Charles Ringera ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (Helb) alisema kuwa majukumu ya shirika la CRB, sio kuwaweka watu kwenye “orodha nyeusi” bali ni kuweka rekodi za alama za mikopo.

“Alama za mikopo ni muhimu kwa taasisi zinazotoa mikopo ili kuwawezesha kufanya uamuzi wa kiwango cha mkopo kinachoweza kutolewa kwa kila mtu,” alisema Bw Ringera.

Hii inajiri wakati taasisi zinazotoa mikopo mitandaoni ikiongezeka kila siku.

You can share this post!

Kifo cha diwani wa Kahawa Wendani chaacha wengi na mshangao

Janga la moto ladhibitiwa Australia

adminleo