• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Serikali yalaumiwa kusaliti Mau Mau, familia ya Kimathi

Serikali yalaumiwa kusaliti Mau Mau, familia ya Kimathi

Na NICHOLAS KOMU

WAHANGA wa Mau Mau pamoja na familia ya Dedan Kimathi sasa watafuatilia haki kivyao baada ya kuhisi kusalitiwa na taifa lao wenyewe.

Bw Dedan Kimathi alitambuliwa kama shujaa wa kitaifa mnamo 2007 lakini serikali haijajishughulisha vya kutosha kumpa heshima au familia yake.

Katika kinachoonekana kama kinaya, serikali imeruhusu tu kutolewa kwa faili za kesi ya Kimathi lakini suala kuhusu mahali ambapo mwili wake ulizikwa likiepukwa kabisa.

Huku wakiadhimisha jana miaka 63 tangu mpiganiaji uhuru huyo alipouawa, wahanga wa Mau Mau wanahisi kutelekezwa, kusalitiwa na kudanganywa.

Walikuwa wakizungumza katika Shule ya Upili ya Dedan Kimathi Memorial mjini Nyeri ambapo mpiganiaji uhuru huyo alikuwa akihudumu kama mwalimu kabla ya vita vya Mau Mau kuanza katika miaka ya 1950.

Akilalamika kwa uchungu, Bi Evelyn Wanjugu, bintiye Dedan Kimathi, aliishutumu serikali dhidi ya kudanganya familia hiyo na kulemaza juhudi za kuwapatia ardhi wahanga wa Mau Mau.

“Tumechoka kusalitiwa na kudanganywa na serikali ya Kenya kwa zaidi ya miaka 60. Nina machungu mno kwa sababu mamangu yuko karibu kufa na hajaruhusiwa kumzika baba yetu. Mtu asikudanganye, hakuna anayependa au kuheshimu Mau Mau,” alisema.

You can share this post!

JSC yakutana kusaka mrithi wa Maraga

Supkem kutoa orodha ya maajenti wa safari za kwenda Hija

adminleo