• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Mahakama yaombwa iapishe majaji 41

Mahakama yaombwa iapishe majaji 41

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAHARAKATI Adrian Kamotho Njenga, anaomba Mahakama Kuu imruhusu Jaji Mkuu David Maraga kuwaapisha majaji 41 walioteuliwa na Tume ya Uajiri wa Idara ya Mahakama (JSC) mwaka uliopita.

Katika kesi aliyowasilisha chini ya ombi la dharura, Bw Njenga anaomba mahakama ishurutishe kuapishwa kwa majaji hao 41 baada ya uamuzi wa korti mnamo Februari 6, 2020.

Majaji hao waliteuliwa Julai mwaka 2019 na majina yao kupelekewa Rais Uhuru Kenyatta.

Bw Njenga anaomba mahakama itoe maagizo ikimshurutisha mwanasheria mkuu achapishe majina ya majaji hao 41 katika muda wa siku tatu.

Anasema kwamba maagizo ya Majaji Lydia Achode, Enoch Mwita na James Makau yamepuuzwa na Rais Kenyatta.

Majaji hao walimwamuru Rais Kenyatta awaapishe majaji hao katika muda wa siku 14 kuanzia Februari 6, 2020.

Bw Njenga anasema muda wa siku 14 umeyoyoma.

You can share this post!

FORT JESUS: Historia, utamaduni, utalii, sanaa na utafiti

Rais aahidi kutekeleza mapendekezo ya sukari

adminleo