• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
CORONA: Wauzaji miraa wakemea marufuku

CORONA: Wauzaji miraa wakemea marufuku

Na DAVID MUCHUI

WAFANYABIASHARA wa miraa wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na kusitishwa kwa biashara ya miraa eneo hilo huku wakikanusha ripoti kwamba, Somalia imepiga marufuku uuzaji wa zao hilo kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wauzaji Miraa Nyambene (Nyamita) Kimathi Munjuri alimkosoa Gavana wa Mandera Ali Roba na mwenzake wa Makueni, Kivutha Kibwana kwa kupiga marufuku biashara ya miraa katika kaunti zao.

Wawili hao walitaja tishio kuu la usambazaji wa virusi vya corona kupitia kushika bidhaa hiyo ambayo kwa kawaida hutafunwa.

Isitoshe, Bw Munjuri aliwalaumu wanaharakati dhidi ya matumizi ya miraa kwa kueneza ripoti kwamba Somalia ilikuwa imesitisha uagiziaji nchini wa miraa kufuatia kuthibitishwa kwa virusi vya corona nchini humo.

Baadhi ya vyombo vya habari jana viliripoti kwamba wizara ya usafiri nchini Somalia ilikuwa imesitisha uagiziaji nchini wa miraa kutoka Kenya na Ethiopia kutokana na mkurupuko wa Covid-19.

 

You can share this post!

Thiwasco yashirikiana na kaunti kuweka vituo vya usafi Thika

Mafuriko yatatiza wakazi wa Nyando na Taita Taveta corona...

adminleo