• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
Wauguzi wataja nyenzo muhimu kwao kukabiliana na Covid-19

Wauguzi wataja nyenzo muhimu kwao kukabiliana na Covid-19

Na MAGDALENE WANJA

MWENYEKITI wa muungano wa wauguzi nchini Kenya Bw Alfred Obengo ametaja kuwaandaa na kuwapa vifaa muhimu wahudumu wa afya kama njia mojawapo ya kuwapa ujasiri kupigana na Covid-19.

Kulingana na Bw Obengo,kuwaandaa wahudumu wa afya pia ni muhimu katika kuhakikisha kwamba hawatapata maambukizi wakitoa huduma kwa wagonjwa hao.

“Ni muhimu pia kwa wauguzi na wahudumu wengine wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa walioambukizwa kupewa bima ya kipekee pamoja na posho ya juu zaidi yaani enhanced allowance,” amesema Bw Obengo.

Hata hivyo, Bw Obengo amesema kuwa muungano huo umeridhishwa na jinsi ambavyo serikali imejitolea kupigana na kuzuia maambukizi ya maradhi hayo.

“Ni jukumu la kila mtu kufuata sheria zilizowekwa na serikali kama njia ya kujikinga dhidi ya maambukizi,” ameongeza Bw Obengo.

Kufikia sasa, visa saba vya virusi vya corona vimeripotiwa nchini.

You can share this post!

Linah Anyango ateuliwa kuwania tuzo ya mwalimu bora duniani

Wanajeshi wa KDF waua al-Shabaab 12 na kumkamata mmoja...

adminleo