• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Mikakati zaidi kukabili virusi vya corona kutolewa

Mikakati zaidi kukabili virusi vya corona kutolewa

Na SAMMY WAWERU

MIKAKATI zaidi kudhibiti usambaaji wa Covid-19 hapa nchini itatolewa hii leo, Jumatano.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema hiyo ndiyo njia pekee kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo hatari vya corona.

“Kwa sasa kuna mikutano kadhaa inaendelea, kesho (Jumatano) tutatoa mikakati zaidi,” Bw Kagwe akasema Jumanne wakati akihutubia kikao cha wanahabari Afya House jijini Nairobi.

Kufikia Jumanne, watu tisa zaidi walikuwa wameripotiwa kuambukizwa Covid-19, takwimu za wenye virusi hivyo nchini zikifikia jumla ya watu 25.

Kati ya tisa hao, Waziri alisema saba ni raia wa Kenya. Alisema visa hivyo vipya vilikaguliwa na kuthibitishwa kutoka kaunti ya Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale, kaunti alizotaja kwamba zimeathirika pakubwa.

Waziri pia alisema wagonjwa wa Covid-19 wametengwa na wanaendelea kupata matibabu. Aliongeza kusema kuwa serikali inaendelea kusaka waliotangamana na wagonjwa hao.

Kufikia Jumanne, jumla ya watu 745 walikuwa wamebainika kutangamana na wathiriwa, kati yao 98 wakiruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kukamilisha kipindi cha siku 14 cha karantini.

Huku taifa likisubiri mikikati zaidi kutolewa, inahofiwa huenda serikali ikaamuru biashara zote zifungwe ili kudhibiti usambaaji wa Covid-19. Mnamo

Jumapili, baa, maeneo ya burudani na makanisa yote yaliamriwa kufungwa mara moja.

You can share this post!

Aachiliwa baada ya kuishi rumande siku 15

Mitumba yapigwa marufuku

adminleo